Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade), Edwin Rutageluka (mwenye suti waliokaa) akiwa pamoja na Wafanyakazi wa Viwanda Vidogo (SIDO) kwenye banda lao katika Maonesho ya Pili ya Sido Kitaifa 2019 yanayofanyika mkoani Singida.
Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (Tantrade) Edwin Rutageluka akizungumza na wafanyakazi wa Sido katika maonesho hayo.
Muonekano wa sehemu ya mabanda katika maonesho hayo.
Mjasiriamali Prudent Sulle (kushoto) kutoka Kampuni ya Rose Products ya Jijini Mwanza, akitoa maelezo kwa wananchi waliotembelea banda lao kuhusu bidhaa zao wanazo zizalisha. Kutoka kulia ni Kapande Noni, Ambros Msimbe na Mkurugenzi wa Kampuni hiyo, Rose Stephen.
Frank Lyakurwa kutoka Dar es Salaam (kulia) akielekezwa jambo na Afisa Mauzo wa Benki ya NMB, Michael Mwangamila baada ya kufungua akaunti ya chapuchapu katika maonesho hayo. Kutoka kushoto ni Wakala wa Benki hiyo, Nathan Nzolo na Afisa wa Benki hiyo Suzan Peter.
Mkaguzi wa Ndani wa Benki ya NMB Mkoa wa Singida, Eliazary Lwanji akitoa maelezo kwa wananchi waliotembelea banda lao katika maonesho hayo.
Afisa Vipimo Mwandamizi wa Wakala wa Vipimo, Wilue Amos akitoa maelezo kwa wananchi waliotembelea banda lao kuhusu kifaa cha kupimia pampu za mafuta kinavyofanya kazi. Wa pili kulia ni Katibu Mahsusi (PS) wa Wakala wa Vipimo Mkoa wa Singida, Grace Severe.
Afisa kutoka Kampuni ya Helvetas Tanzania, John Mabagalu (kulia) akitoa maelezo kwa Mkazi wa Magu Mwanza, Juma Kisinza kuhusu mchele unaozalishwa na kampuni hiyo ambao unatumiwa na watu wenye kisukari.
Afisa Mawasiliano na Mahusiano ya Umma wa Tume ya Ushindani ( FCC) Adefrida Ilomo akionesha bidhaa zisizo na ubora zilizotengenezwa kinyume cha sheria.
Mwelimishaji Kodi kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Mkoa wa Singida, Japhary Hamisi akitoa maelezo kwa Mjasiriamali Nancy Kimalila aliyetembelea banda lao.
Joseph Kavishe, akijieleza kwa Afisa wa Benki ya CRDB, Evance Makundi (kushoto) alipotembelea banda la Benki hiyo katika maonesho hayo. Katikati ni wakala wa CRDB, Maria Kitima.
Wafanyakazi wa Kituo cha Radio cha Standard FM cha Mjini Singida, Ally Juma na Faida Adam wakiwa mbele ya banda lao katika maonesho hayo.
Afisa wa Benki ya Biashara Tanzania (NBC) Suzan Zoya (kulia) akimuelekeza jambo Mzee Samson Mweru alipotembelea banda la Benki hiyo.
Wafanyakazi wa Benki ya NMB Mkoa wa Singida wakiwa kwenye banda lao.
Banda la Benki ya Biashara ya NBC kwa ajili ya kutolea mafunzo ya biashara lililopo katika maonesho hayo.
Afisa wa Kampuni ya Faida Mali, Irene Njovu akimuelekeza Mzee Joseph Hoyanga jinsi mashine ya kupima ubora wa vyakula inavyofanyakazi. Kulia ni Afisa wa Kampuni hiyo, Peter Charles.
Afisa wa Kampuni ya Faida Mali, Lazaro Mnkumbu (katikati) akitoa maelekezo jinsi ya kutumia mashine ya kupandia mbegu zinazosambazwa na kampuni hiyo. Kulia ni Mzee Masegense Masegense na Ramadhani Makenya.
Afisa wa Benki ya Tpb Bank, Lilian Rutha akitoa maelezo kwa Mtaalamu wa Kilimo, Mashaka Mlangi alipotembelea banda la Benki hiyo.
Afisa Maendeleo ya Jamii wa Kijiji cha Mpandangendo Mkoa wa Ruvuma kutoka Shirika la Maendeleo la Japan (JICA) Ryuta Okamoto akionesha wananchi jinsi ya kutumia kibao maalumu cha kufulia nguo pamoja na kifaa cha kupukuchulia mahindi kilichotengenezwa na vijana kutoka katika kijiji hicho waliopatiwa mafunzo na shirika hilo.
Afisa Uhusiano wa Benki ya Biashara (NBC) Mkoa wa Singida, Ally Idd (kushoto) akimsikiliza Mdhibiti Ubora wa Elimu wa Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA) Tawi wa la Singida, Daniel Mgonja alipotembelea banda la Taasisi hiyo. Katikati ni Mhadhiri Msaidizi wa Taasisi hiyo Mkoa wa Singida, Eliaichi Kyara.
Watoto wakipata burudani ya kubembea katika maonesho hayo kwa gharama ya sh.1000 kwa dakika nane.