Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akipokea taarifa ya mradi wa maji wa Kintiku |
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akisalimiana na viongozi mbalimbali wa Mkoa wa Sindida. |
Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Manyoni wakiwa katika mkutano wa Waziri Mkuu.
Mkuu wa Mkoa wa Singida, Dkt.Rehema Nchimbi akizungumza.
Mbunge wa Jimbo la Singida Mashariki, Daniel Mtuka akizungumza kwenye mkutano wa ndani wa Waziri Mkuu na watumishi wa Umma.
Mbunge wa Manyoni Magharibi, Yahaya Masare akizungumza.
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira ambaye ni Mbunge wa Singida Mjini, Mussa Sima akizungumza.
Mbunge wa Viti Maalumu (CCM) Mkoa wa Singida, Aysharose Mattembe akizungumza.
Watumishi wa Umma kutoka Wilaya ya Itigi na Manyoni wakiwa kwenye mkutano huo.
Katibu wa CCM Mkoa wa Singida Alexandrina Katabi akimkabidhi Waziri Mkuu Kassim Majaliwa taarifa ya chama ya mkoa huo.
Na Dotto Mwaibale, Manyoni
WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa ameitaka Halmashauri ya Wilaya ya Itigi kurejesha sh.100.9 milioni zilizotengwa na Serikali kwa shughuli maalumu ambazo halmashauri hiyo
ilibadilisha matumizi yake.
Katika hatua nyingine amemtaka Kaimu Mweka Hazina wa Halmashauri hiyo Likilimke Otto kureshesha sh.milioni 1.6 alizolipwa kama posho za kwenda Dodoma kikazi ambapo pia
amemwagiza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Manyoni Charles Fussi kupeleka sh.100 milioni Benki ya CRDB wilayani humo zilirejeshwa na madiwani baada ya kupewa mkopo na
benki hiyo lakini hajazipeleka na riba yake kuwa kubwa.
Waziri Mkuu alitoa maagizo hayo wilayani Manyoni katika siku yake ya kwanza ya ziara ya kikazi mkoani Singida wakati akizungumza na watumishi wa wilaya hiyo leo.
“Kuna fedha tulizileta katika Halmashauri yenu ya Itigi sh.100.9 lakini mmezibadilisha matumizi nataka mzirejeshe na wewe mweka hazina nataka mpaka siku yangu ya mwisho ya
ziara uniletee stakabadhi za malipo ya kurejesha fedha hizo” alisema Majaliwa.
Majaliwa aliwata watumishi wa umma kuacha kukaa ofisini badala yake watumie siku tatu za wiki kwenda kuzungumza na wananchi ili kujua kero zao na kutafutiwa ufumbuzi.
Alizitaka halmashauri zote nchini kutafuta vyanzo vya mapato na kutumia fedha hizo kwa miradi mikubwa badala ya kusubiri fedha kutoka serikali kuu.
Majaliwa alitumia nafasi hiyo kwa kuipongeza Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi kwa kusimamia vizuri fedha za miradi zinazotolewa na serikali.
Katika ziara hiyo wilayani Manyoni aliweza kukagua ujenzi wa mradi mkubwa wa maji wa Kintiku Lusilile, shamba la korosho la Misigati na Katika wilaya ya Itigi kuweka jiwe la
msingi la jengo la ofisi ya halmashauri hiyo.