Upepo uliovuma jana Ghafla katika mkoa wa Arusha umesababisha kuzama kwa watalii wawili katika ziwa momela katika hifadhi ya taifa ya Arusha iliyopo katika wilaya ya Arumeru kufuatia mtumbwi waliokuwa wanautumia kutalii katika ziwa momela kupigwa na Dhoruba ya upepo na kupinduka majira ya jana mchana.
Juhudi za kuokoa watu hao zimewezesha kupatikana kwa mtalii mmoja Raia wa nje
Jitihada zinaendelea kumtafuta kijana aliezama ambae aliekuwa akimuongoza mtalii huyu (tour guide) ambae alizama baada ya mtumbwi kupinduka.
Mkuu wa wilaya ya Arumeru Ndugu Jerry Muro na timu ya uokozi kutoka kikosi cha zimamoto na uokoji wanaendelea kumtafuta kijana