NA:ELISA SHUNDA,IRINGA
MAKATIBU Wakuu wa Jumuiya za Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wametembelea Chuo cha Mafunzo ya Itikadi,Uenezi na Uzalendo cha Ihemi Kilichopo Kata ya Mgama wkoani Iringa katika Halmashauri ya Iringa Vijijini Kujionea Maboresho ya Miundombinu katika Chuo Hicho Ambacho Kitakapokamilka Kitajishughulisha na Masuala Mbalimbali Ikiwemo Mafunzo ya Kilimo Bora,Ushonaji,Ufugaji wa Samaki,Ufugaji wa Nyuki Pamoja na Utalii katika Sehemu Maalumu Itakayotengwa.
Akizungumza, Jana, Baada ya Kuwapokea Viongozi Hao katika Chuo cha Ihemi,Katibu wa Uchumi na Fedha wa Umoja wa Vijana wa CCM Taifa,Lusekelo Nelson, Alisema Kuwa Kwa Chuo Hicho cha Ihemi Kimeanza na Mradi wa Green House Ambapo Tayari Wameshajenga Vitalu Nyumba Vitatu,Ujenzi Wake Ulihusisha Mafunzo ya Vijana Mia tatu katika Kujenga na Kupanda Nyanya kwa Njia ya Kisasa.
“Mategemeo Yetu Kwa Taarifa Tuliyopewa na Wataalamu wa Kilimo cha Kisasa Walituambia Kitalu Nyumba Kimoja (Green House) Kwa Msimu Kinatoa Tani Saba na Kwa Vitalu Nyumba Mia Moja Tutazalisha Tani Mia Saba Ambazo Sisi kwa Malengo Yetu Ndani ya Miaka Mitano Ijayo Tutakuwa Tuna Uwezo wa Kupata Shilingini Bilioni nne kwa Mwaka,Pia Tuna Mradi wa Nyuki Mizinga Laki Moja Tutaanza na Mafunzo Yake” Alisema Lusekelo.
Aidha Lusekelo Alisema Katika Eneo Hilo Wana Shamba Walilotenga la Ekari 600 Ambalo Litakuwa Maalumu kwa Utalii wa Wanyama Pori Ambao ni Rafiki Wasio na Madhara Kama Swala,Pundamilia,Twiga,Kobe na Wanyama Wengine Wapore,Wanyama Watakaozidi Kulingana na Idadi Inayotakiwa Hapa Tutawauza Kwa Kufuata Sheria na Sera ya Ufugaji Wanyama Inavyosema.
Kwa Upande wa Katibu Mkuu Uvccm,Mwalimu Raymond Mwangala, Alisema Lengo la Kufika katika Chuo Hicho Akiwa Pamoja na Viongozi Wenzake wa Jumuiya ya Wazazi na Uwt ni Kuja Kuangalia Fursa ya Kuwekeza kwa Kuwa Eneo Hilo ni Mali ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Kijana Atakayepita katika Chuo Hicho Atakwenda Kuwa Msaada Kwa Jamii Atakayokwenda Kuishi Nayo Akiwa Amepata Mafunzo ya Uadilifu na Mapenzi ya Kuipenda na Kuijali Nchi Yake.
“Kijana Yeyote Atakayepitia katika Chuo Hiki Ukiachia Mafunzo ya Ujasiliamali Atakaopata lakini Pia Ataondoka na Faida ya Mafunzo ya Uzalendo,Upendo na Afrika Yake,Umoja kwa Wenzake Pamoja na Kuilinda Nchi Yake Abayo Yeye na Ndugu Zake Wanaishi Asiwe Mshabiki wa Masuala Yasiyo na Tija kwa Taifa” Alisema Mwangala.
Katibu Mkuu wa Umoja wa Wazazi Tanzania Jumuiya ya CCM,Erasto Sima, Aliwapongeza Uvccm kwa Usimamizi wa Chuo Hiko kwa Jinsi Kinavyoboreshwa, Kwa Upande wa Jumuiya ya Wazazi Kupitia Mkoa wa Iringa Tayari Wameweka Mizinga 21 Kama Sera ya Muongozo wa Jumuiya Ulivyotoa Tamko Ngazi Zote Kujishughulisha na Mradi Huo.
Kuhusu Vitalu Nyumba (Green House),KATIBU Mkuu,Sima,Alisema Watafanya Jitihada ya Kuhamasisha katika Maeneo Mengine Kujenga Ili Nao Wanufaike.
“Tutaangalia Uwezekano wa Kuileta Kamati ya Utekelezaji Taifa au Baraza Kuu la Wazazi Taifa Waje Wajifunze Ili Wakiondoka Hapa Wakatekeleze katika Mikoa na Wilaya Zao Ili Elimu Hiyo Isambae Nchi Nzima”Alisema Sima.
Katibu Mkuu wa Uwt,Mwalimu Queen Mlozi, Aliipongeza Jumuiya ya Vijana Chini y’a Mtendaji Wake Mkuu,Mwangala Kupitia Chama Kwa Maboresho ya Miundombinu Inayofanyika Chuoni Hapo, Alisema Wao Kama Jumuiya ya Wanawake ndani ya CCM Watahakikisha Wanatumia Vizuri Fursa Zitakazokuwa Zikipatikana Kwenye Chuo Hicho.