Mbunge wa Jiambo la Kibaha Vijijini Hamoud Jumaa kushoto akikabidhiwa zawadi ya fimbo na mmoja wa viongozi wa jamii ya wafugaji alipowasili katika kijiji cha Kigoda, kulia kwake ni Naibu waziri wa elimu sayansi na teknolojia William Ole Nasha baada ya kuwasili katika eneo hilo kwa lengo la kuweka jiwe la msingi katika ofisi ya kijiji hicho pamoja na kutembelea eneo ambalo limetengwa kwa ajili ya ujenzi wa shule ya kata (PICHA NA VICTOR MASANGU)
Naibu waziri wa elimu sayansi na teknolojia wa kati kati akipiga makofi katika halfa ya uwekaji wa jiwe la msingi katika ofisi ya kijiji cha kigoda kilichopo kata ya Gwata katika halmashauri ya Kibaha vijini kushoto kwake ni Mbunge wa Kibaha Vijijini Haoumd Jumaa, na viongozi wengine wa kijiji hicho.(PICHA NA CICTOR MASANGU)
Naibu waziri wa elimu William Ole Nasha kushoto akiwa katika halfa ya uwekaji wa jiwe la msingi pamoja na kutembelea eneo la ambalo limetengwa kwa ajili ya mradi wa ujenzi wa shule mpya ya kata ya Gwata.kulia kwake ni Mbunge wa Jimbo la Kibaha vijijini Haoumd Jumaa.(PICHA NA VICTOR MASANGU).
Mbungewa Jimbo la Kibaha vijijini Haoumd Jumaa akizungumza na baadhi ya wananchi wa kata ya Gwata hawapo pichani wakati wa sherehe za uwekaji wa jiwe la msingi katika mradi wa ujenzi kwa ajaili ya ofisi ya kijiji cha kigoga pamoja na kujoinenea eneo ambalo limetengwa kwa ajili ya ujenzi wa shule ya kata(PICHA NA VICTOR MASANGU).
***********************************
NA VICTOR MASANGU, PWANI
Naibu Waziri wa elimu sayansi na teknolojia Williamu Ole Nasha amechukizwa kuona vitendo vya baaadhi ya wazazi wa jamii ya wafugaji kutothamini suala la elimu na kuamua kuwaozesha watoto wao mapema na kuwatumikisha katika kazi za kuchunga mifugo ambapo amekemea na kulaani vikali vitendo hivyo na kuwataka kuhakikisha wanawapeleka watoto wao shule ili kuunga mkono juhudi za serikali ya awamu ya tano katika sekta ya elimu ikiwemo utoaji wa elimu bure..
Ole Nasha ametoa kauli hiyo wakati wa halfa ya uwekaji wa jiwe la msingi katika mradi wa ujenzi wa ofisi ya serikalI ya kijiji cha Kigoda kilichopo katika kata ya Gwata Wilaya ya Kibaha sambamba na kutembelea eneo maalumu ambalo limetengwa kwa ajili ya ujenzi wa shule ya sekondari ya kata ambayo itaweza kuwa mkombozi mkubwa kwa wanafunzi ambao wamekuwa wakitembea umbari wa kilometa nane kwenda kutafuta huduma ya elimu katika maeneo mengine.
Aliongeza kuwa lengo la serikali ya awamu ya tano ni kuboresha sekta ya elimu katika ngazi zote hivyo kitu kikubwa ni kuhakikisha watoto wanapatiwa malezi bora ikiwemo kuwapeleka shule lengo ikiwa ni kuwapatia ujuzi na mahalifa ambao utaweza kuliletea taifa maendeleo.
“Nampongeza sana Mbunge wa jimnbo la Kibaha Vijijini kwani amekuwa ni mtu mwenye kunisumbua sana lakini lengo lake kubwa ni kuwaletea maenedeleo wananchi wake, kwa hiyo kikubwa zaidi tumuunge mkono katika kuleta mabadiliko na hili tabia ya kuwaozesha watoto wenu kwa kweli mimi nataka muiache kabisa na kuwachungisha ng’ombe,”alisema.
Mmoja wa wazazi wa jamii ya wafugaji akizungumza kwa niaba ya wenzake aliahidi kulitekeleza na kulivalia njuga agizo ambalo limetolewa na Naibu Waziri na kwamba wataweka mipango madhubuti ya kuwapatia watoto wao haki zao za msingi ikiwemo kuwapeleka shule pamoja na kuachana na tabia ya kuwatumiksiha kwa kipindi kirefu katika kuchunga
Naye Mbgunge wa Jimbo la Kibaha vijijini Hamoud Jumaa katika kuunga juhudi za Rais wa awamu ya tano Dk. John Pombe ,Magufuli katika sekta ya elimu ameamua kutoa eneo la hekari kumi pamoja na kuahidi ujenzi wa madarasa mawili kwa lengo la kuanzisha mradi wa ujenzi wa shule ya kata ya Gwata ambayo itapunguza kwa kiasi kikubwa adha na kero kwa wanafunzi ambao wamekuwa wakitumia muda wao mwingi wakiwa njiani kuelekea shuleni.
“Kwanza kabisa napenda kumpongeza Naibu waziri wa elimu kwa kuja kufanya ziara katika kijiji hiki na mimi napenda kumuahidi kuwa maelekezo yake yote ya kuongeza hekari zingine mimi nipo tayari kwa hiyo mimi ninatongeza hekari zingine tano kwa hiyo jumla zitakuwa kumi hii yote ni kuhakikisha tunaunga mkono juhudin za serikali ya awamu ya tano katika kuboresha elimu,”alisema Jumaa.
Aidha Jumaa katika hatua nyingine amesema lengo lake kubwa ni kuhakikisha kwamba analeta mabadiliko chanya ya kimaendeleo katika Nyanja mbali mbali na kwamba atashirikiana bega kwa bega na wananchi pamoja na serikali kwa jili ya kukamilisha mradi wa ujenzi wa shule hiyo ya kata ya Gwata ambayo itakuwa ni msaada mkubwa katika kuwaondolewa wanafunzi changamoto ya kutembea umbari mrefu.
Pia aliwaasa wazazi na walezi wa jamii ya wafugaji kumuunga mkono Rais wa awamu ya tano Dr.John Pombe Magufuli katika kuhakikisha kwamba watoto wote wenye umri wa kwenda shule wanapelekwa mara moja ili kuwapatia haki yao ya msingi pamoja na kuwataka kuachana na tabia ya kuwakatisha masomo bila sababu zozote za msingi.
KUMEKUWEPO na wimbi la baadhi ya jamii ya wafugaji katika Wilaya ya Kibaha Mkoani Pwani kuamua kuwakatisha watoto wao masomo na kuwatumikisha katika kazi mbali mbali ikiwemo kuwapeleka maporini kwa ajili ya kuchunga ng’ombe na mbuzi pamoja na wengine kuwaozesha kitu ambacho kinawanyima kupata haki zao za msingi ikiwemo suala la elimu.