Home Mchanganyiko Wananchi Wilaya ya Chemba katika mkoa wa Dodoma waiomba Serikali kuiangalia wilaya...

Wananchi Wilaya ya Chemba katika mkoa wa Dodoma waiomba Serikali kuiangalia wilaya hiyo kwa jicho la huruma

0

Mwakilishi wa wananchi hao akisoma risala kwa mgeni rasmi Hamisi Mktoya ambaye ni mdau wa maendeleoMwakilishi wa wananchi hao akisoma risala kwa mgeni rasmi Hamisi Mktoya ambaye ni mdau wa maendeleo

Wananchi wa Wilaya ya Chemba waishio jijini Dar es Salaam wakiwa katika mkutano wa kuzungumzia maendeleo pamoja na kutoa kero za Wilaya hiyo na hasa Kata za Farkwa na Kwa Mtoro

Wananchi wa Tarafa za Farkwa na Kwa Mtoro wakifuatilia majadiliano wakati wa kikao chao cha kujadili maendeleo kilichofanyika jijini Dar es Salaam

Baadhi ya wananchi waliohudhuria mkutano huo wakisiliza hoja mbalimbali kutoka kwa wachingiaji waliopata nafasi ya kuzungumzia maendeleo ya Wilaya ya Chemba na hasa tarafa za Farkwa na Kwa Mtoro

Mdau wa Maendeleo Hamisi Mkotya akifafanua jambo mbele ya wananchi wa Wilaya ya Chemba wanaoishi Dar es Salaam .Wananchi hao.ambao ni Wasandawe wanatoka katika Tarafa za Kwa Mtoro na Farkwa

Mdau wa Maendeleo kutoka Wilaya Chemba mkoani Dodoma Hamisi Mkotya akizungumza kwenye mkutano wa wananchi wa kabila la Wasandawe kutoka Wilaya ya Chemba waishio jijini Dar es Salaam ambapo walikutana kuzungumzia changamoto zilizopo ndani ya Wilaya hiyo.Mkotya ndio aliyekuwa mgeni rasmi wakati wa kikao hicho kutokana na wananchi hao kutambua mchango wake kwenye maendeleo

………………………………………………

WANANCHI wa Wilaya ya Chemba katika Jiji la Dodoma wameiomba Serikali ya Awamu ya Tano kuiangalia wilaya hiyo kwa jicho la huruma kwa lengo la kuboresha huduma muhimu za kijamii ndani ya wilaya hiyo.

Wakizungumza katika mkutano wa wananchi hao kutoka tarafa ya Farkwa na Kwa Mtoro wilayani Chemba wananchi hao ambao ni wa kabila la Wasandawe ambao wanaishi katika Jiji la Dar es Salaam wametumia mkutano wao kujadili masuala mbalimbali yanayohusu wilaya yao na hasa walijikita katika kuzungumzia mafanikio na changamoto.
Wamesema kuwa ni kweli wao wanaishi Dar es Salaam kwa sasa lakini wanakotoka ni Wilaya ya Chemba katika tarafa hizo za Farkwa na Kwa Mtoro, hivyo wanalo jukumu la kukutana na kuzungumza mustakabali wa tarafa hizo na Wilaya ya Chemba kwa ujumla kwani iko siku nao watarudi kijijini.
Katika mkutano huo wananchi hao walikuwa wamewalika vingozi mbalimbali huku mgeni rasmi akiwa Mdau wa Maendeleo wa Wilaya ya Chemba Hamisi Mkotya ambaye pia ni Mwandishi wa habari wa siku nyingi ambaye amekuwa akitumia taaluma yake ya habari na kalamu yake kueleza mazuri ya Wilaya ya Chemba na kushiriki kikamilifu katika maendeleo ya wananchi hao.
Akizuzungumza katika mkutano huo Mkotya ambaye pia ni mzaliwa wa Wilaya ya Chemba ametumia nafasi hiyo kuzungumza na wananchi hao na kubwa zaidi ambalo amewashauri ni kuwa bega kwa bega katika kushirikiana na Serikali kutafuta ufumbuzi wa changamoto na kuongeza kwamba Serikali ya Awamu ya Tano imejikita kusaidia wananchi wanyonge, hivyo ni matumaini yake kilio chao kitasikika.
Mdau wa maendeleo ya Wilaya ya Chemba,ameiomba Serikali kusikia kilio cha wananchi hao kwa kuwaboreshea huduma za kijamii huku akitumia nafasi hiyo kuwashauri kujenga utamaduni wa kwenda kuwekeza nyumbani kama hatua ya kujiletea maendeleo, kwani Chemba itajengwa na wanachemba wenyewe.

Amefafanua kuwa kuna mradi wa ujenzi wa Bwawa la Farkwa ambao ukikamilika utasaidia kupunguza kero ya maji katika wilaya hiyo ambayo inakabiliwa na tatizo la ukosefu wa maji ikiwamo tarafa za Mondo na Goima na kuongeza kuwa Chemba ni miongoni mwa wilaya zenye fursa nyingi za kiuchumi, lakini bado ipo nyuma kimaendeleo.

Awali baadhi ya wananchi wakizungumza kwenye mkutano huo wametumia nafasi hiyo kueleza changamoto zilizoko ikiwemo ya uhaba wa maji, ubovu wa miundombi ya barabara ndani ya tarafa hizo pamoja na barabara nyingine za Wilaya na huduma za afya ambapo wameiomba Serikali kuangalia namna ya kuzitafutia ufumbuzi wake ,huduma za afya pamoja na uhaba wa vifaa vya kua wilaya kwa

Mmoja ya wananchi hao Hamisi Waziri amesema kuwa kwa sasa wanaishi Dar es Salaam ambako kuna kila kitu kuanzia barabara nzuri, huduma bora za afya, maji safi na salama pamoja na lakini watambue kuna siku watarudi Chemba, hivyo wanaweka mazingira gani ya kuhakikisha nako kunakuwa na maendeleo.

“Ni haki Watanzania kokote waliko wanahaki ya kupata muhimu za kijamii na ndio maana wamekutana kujadili maendeleo ya Wilaya ya Chemba na Mkoa wao kwa ujumla.

“Dhumuni la kukutana ni lile lile la kutatua matatizo mbalimbali kama ambavy tunajua kwenye vikundi vyetu vya Wana Chemba na ndivyo hivyo hivyo ambavyo tumekutana leo katika mkutano huu Wasandawe tunaoishi jijini Dar es Salaam.Kufanya jambo nzuri kwa ajili ya Chemba hatuna sababu ya kuiachia Serikali, bali nasi tunawaojibu huo kwa umoja wetu,”amesema.

Hata hivyo amesema wanatamani kuona Rais Dk.Magufuli anafanya ziara kwenye Wilaya ya Chemba, na kwamba ili afike wao wanalo jukumu la kutoa kero zao ambazo wanaamini zitamfikia Rais na kufanyiwa kazi.

“Katika mkutano huu ambao umetukutanisha wananchi wengi ni rahisi tutakayosema kusikika.Kwetu sisi tunaomba tu kuboreshewa huduma za kijamii ambazo ni muhimu, tunachangamoto nyingi na kwa bahati mbaya kuna baadhi ya viongozi walioko kwenye Wilaya yetu si wakweli katika kuzungumzia maendeleo,”amesema Waziri