Home Mchanganyiko BASHE AWATAKA MAAFISA UGANI KUTUMIA FOMU MAALUM KUKUSANYA TAARIFA ZA WAKULIMA

BASHE AWATAKA MAAFISA UGANI KUTUMIA FOMU MAALUM KUKUSANYA TAARIFA ZA WAKULIMA

0

Waziri wa kilimo Mhe.Hussein Bashe  akielezea hoja mbalimbali zinazoikabili sekt ya kilimo

Waziri wa kilimo Mhe.Hussein Bashe akiwa kwenye kikako kilichofanyika katika ukumbi wa mikuutano wa mkuu wa mkoa leo wajadili zoezi na unauazi wa pamba

Waziri wa kilimo Mhe.Hussein Bashe akipata maelezo kutoka kwa  Mkuu wa Mkoa Bi Zainabu Telaki 

Waziri wa kilimo Mhe.Hussein Bashe alipomkabidhi Mkuu wa Mkoa Bi Zainabu Telaki fomu itakayotumika kukusanyia taarifa muimu za wakulima katika halmashauri zote za ukanda unaolima pamba.

****************************

Na Bashiri Salum,Wizara ya kilimo
Shinyanga
01/10/2019

Naibu Waziri wa Wizara ya Kilimo Mhe. Husseni Bashe leo 01.10.2019 amemkabidhi Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Bi Zeinabu Telaki fomu maalumu (call sheet ) ambayo itatumiwa na Maafisa Ugani wakati wa kuwatembelea wakulima na kujaza taarifa zao muhimu zikiwemo namba za simu, aina ya mazao anayolima,mbolea wanayotumia pamoja na changamoto
zinazowakabili .

Akizungumza wakati wa makabidhiano hayo Mhe,Naibu Waziri amesema kwamba Kituo cha Utafiti cha Ukiriguru kitapita kila Halmashauri katika Ukanda wote inapolimwa pamba na kutoa mafunzo kuanzia ngazi ya Maafisa watendaji wa Vijiji ili kusaidia na kushauri shughuli za kilimo ngazi ya chini.

Amesema zoezi hili litaisida kupunguza tatizo la ukosefu wa Maafisa Ugani ambao wangeweza kushauri wakulima.

Aidha amesisitiza kwamba kila Afisa Kilimo wa Kata au Kijiji atatakiwa kutembelea wakulima wasiopungua watano (5) na kuchukua taarifa muhimu zikiwemo majina ya wakulima ukubwa wa shamba, aina ya kilimo kinachofanyika, mbolea iliyotumika mwaka jana na mawasiliano ya
mkulima.

Hata hivyo amemsahuri mkuu wa Mkoa huo kukutana na wenyeviti wa Halmashauri ili kujadili uanzishwaji wa mashamba ya mfano yatakayomilikiwa na Halmashauri hizo ili wakulima waweze kuyatembelea na kujifunza kilimo cha kitaalamu.

Pamoja na mambo mengine Mhe. Bashe amesema umefika wakati ambao zao la pamaba linatakiwa lijitegemee kama yalivyo mazao mengine na serikali imejipanga kuleta viuatilifu kwa wakati na kwa bei nafuu ili wakulima waweze kununua .

Hata hivyo Mhe. Bashe amewatoa hofu wakullima kuhusu upandaji wa bei za mbegu amesema mwaka huu bei haitafika shilingi 1,000 bali itakuwa katika ya sh. 600 na 650 iwe kama namna ya kupunguza machungu ambayo wakulima wa pamba wameyapata kwa mwaka huu.

Amewataka wataalamu wa kilimo kusaidia kuongeza uzalishaji wa pamba kutoka miche 7,000 hadi 20,000 kwa ekari kwa kuwa kutasaidia kuondoa tatizo la bei ya pamba kwa sababu pamba itakuwa nyingi kwa ekari.

Aidha Mhe. Bashe amezishauri Halmashuri nchini kote kujenga maghala kwa ajili ya kuhifadhia mazao ya wakulima baada ya mavuno ili kuondokana na changamoto za mara kwa mara wakati wa mvua.

Naye Mkuu wa Mkoa huo Bi Zainabu Telaki amesema, sasa wameanza jitihada za kuhamia katika kilimo cha umwagiliaji kutokana na uhaba wa mvua katika mkoa huo na kuiomba wizara ya kilimo kusaidia upatikanaji wa miundombinu ya umwagiliaji.

Katika zoezi la ununuzi wa pamba Bi Telaki anasema pamba nyingi ya mkoani kwake imenunuliwa isipokuwa kawma walikuwepo wakulima walioficha majumbania na ile ambayo ilibainika kupenyezwa kinyemela kutoka Mikoa ya jirani wakitafuta soko.

kama kuna pamba iliyobaki "itakuwa ni kidogo sana katika baadhi ya AMCOS na kwa wale ambao walificha ili ipande bei"alisema Bi Telaki
amesema wakulima wengi mkoani humo ikiwemo wilaya ya Kishapu washaanzana kuandaa msimu wa kilimo hivyo amemumba Naibu Waziri kusaidia pembejeo zifike kwa wakati ili wakulima hao wawahi mvua za kwanza.

Awali Mhe. Bashe aliagazi Iadara ya Mazao iliyoko chini ya Wizara ya Kilimo (DCD)kufanya tathmini kwenye sikimu zote katika mkoa huo ili Kujua idadi ya skimu zinazohitaji marekebisho na zinahitaji kujengwa upya.