Home Mchanganyiko Wakazi wa Bukoba waipokea Elimu ya Mpiga Kura kuelekea Uboreshaji wa Daftari...

Wakazi wa Bukoba waipokea Elimu ya Mpiga Kura kuelekea Uboreshaji wa Daftari Oktoba 2-8, 2019

0

Kaimu Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Habari na Elimu ya Mpiga Kura ya Tume ya Taifa ya uchaguzi (NEC) upande wa Habari Daniel Kasokola (katikati ya wanafunzi) akieleza jambo kuhusu watu wenye ulemavu wakati Gari la Matangazo la NEC lilipotembelea Shule ya Sekondari ya Rugambwa iliyopo Manispaa ya Bukoba kutoa Elimu ya Mpiga Kura kuelekea Uboreshaji wa
Daftari la Kudumu la Wapiga Kura kwa mkoa wa Kagera, Kigoma na Wilaya ya Chato unaoanza Oktoba 2 hadi Oktoba 8, 2019.

Kaimu Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Habari na Elimu ya Mpiga Kura ya Tume ya Taifa ya uchaguzi (NEC) upande wa Habari Daniel Kasokola (katikati) akifafanua nafasi ya watu wenye ulemavu katika Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura akiwa na baadhi ya wanafunzi wenye ulemavu wanaosoma Shule ya Sekondari ya Rugambwa ya Manispaa ya Bukoba.

Afisa wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Yasinta Mlula akiwaeleza jambo wakazi wa Manispaa ya Bukoba wakati Gari la Matangazo la Tume lilipokuwa likitoa Elimu ya Mpiga Kura kwenye Stendi ya Mabasi ya Mjini Bukoba kuhusu Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura.

Mkazi wa Manispaa ya Bukoba mwenye ulemavu akiwa na Afisa wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Ibrahim Dedu wakati Gari la Matangazo la Tume (halipo pichani) lilipokuwa likitoa Elimu ya Mpiga Kura kwenye Stendi ya Mabasi ya Mjini Bukoba kuhusu Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura.

Afisa wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Monica Wabukundi, akiwasiliza vijana kwenye Stendi ya mabasi ya Mjini Bukoba wakati Gari la Matangazo la Tume lilipokuwa likitoa Elimu ya Mpiga Kura kwenye stendi hiyo kuhusu Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura.

Picha na Idara ya Habari na Elimu ya Mpiga Kura-NEC