Home Burudani MSIMU WA “MUZIKI MNENE” MWAKA 2019 WAZINDULIWA

MSIMU WA “MUZIKI MNENE” MWAKA 2019 WAZINDULIWA

0

Msafara wa Crew ya EFM na TVE wakielekea katika uzinduzi wa msimu wa MUZIKI MNENE wa mwaka 2019.

Mashabiki waliojitokeza kwa wingi wakifuatilia burudani ya muziki wa Singeri katika uzinduzi wa msimu mpya wa MUZIKI MNENE wa mwaka 2019 katika viwanja vya Tandika Jijini Dar es Salaam.

Crew ya EFM na TVE wakionesha mabango kuashiria ufunguzi wa msimu mpya wa MUZIKI MNENE wa Mwaka 2019.

Crew ya EFM na TVE wakipata picha ya pamoja baada ya ufunguzi wa Msimu wa MUZIKI MNENE wa mwaka 2019 hapo jana katika viwanja vya Tandika Jijini Dar es Salaam.

******************************

NA EMMANUEL MBATILO

Ni mara nyingine tena chombo cha habari na utangazaji cha EFM na TVE wamezindua msimu wa MUZIKI MNENE wa mwaka 2019 kwa dhumuni la kuwawezesha mashabiki wao kuweza kupata vitu vipya na vingine vilivyoboreshwa ikiwemo burudani tosha kutoka kwa wasanii pamoja crow nzima ya EFM na TVE.

Akizungumza katika Uzinduzi huo Mkurugenzi wa uendeshaji wa kituo cha habari na utangazaji cha EFM na TVE, Bw.Dennis Busurwa Ssebo amesema  kuwa baada ya uzinduzi huo watazunguka kwa wiki 12 wakiwa na na mambo mengi kufanya ikiwemo kutakuwa na mchezo wa mpira wa miguu katika maeneo ambayo wataznguka kutangaza msimu huo na pia kutakuwa na jogging kwaajili ya kujiweka sawa kiafya.

Aidha Ssebo ameema kuwa mashabiki wategemee kuona vifaa vya kurushia matangazo vipya na vilivyoboreshwa kwaajili ya kuwapa burudani nzuri mashabiki wao.

Pamoja na hayo Ssebo amesema kuwa changamoto kubwa ambayo huwa wanaipata moja wapo ni sehemu ambayo wanafanyia tukio la uzinduzi wa MUZIKI MNENE kwani mashabiki wengi wamekuwa wakijitokeza kwa wingi kwa kila msimu.