Home Michezo SIMBA HAIKAMATIKI KANDA YA ZIWA YAICHAPA 2-0 BIASHARA UNITED

SIMBA HAIKAMATIKI KANDA YA ZIWA YAICHAPA 2-0 BIASHARA UNITED

0

Na.Alex Sonna,Musoma

Mabingwa wa Ligi Kuu Vodacom Tanzania bara wameendeleza wimbi la ushindi katika mechi zake za kanda ya ziwa  baada ya kupata ushindi wa pili mfululizo.

Simba wameibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya wenyeji timu ya Biashara United mchezo uliopigwa kwenye uwanja wa Karume mjini Musoma.

Mshambuliaji hatari raia wa Rwanda Meddie Kagere aliwanyanyua mashabiki wa Simba kwa kupachika bao safi akimalizia pasi ya Miraji Athumani likiwa bao la sita katika mechi nne.

Hadi timu zinaenda mapumziko Simba walikuwa mbele kwa bao moja ambalo liliweza kuduma kipindi chote cha kwanza.

Kipindi cha pili timu zote zilifanya mabadiliko kwa kuwaingiza wachezaji ambao waliweza kwenda kuongeza nguvu hata hivyo Simba waliweza kunufaika na mabadiliko hayo.

Miraji Athuman aliwanyanyua tena mashabiki wa Simba kwa kufunga bao la kichwa akimalizia mpira wa faulo uliopingwa na Ibrahim Ajibu na kumkutana mfungaji katika sehemu sahihi.

Ushindi huu wa Simba ni wa pili wakiwa kanda ya ziwa baada ya kuifunga Kagera Sugar mabao 3-0 na kwa matokeo hayo wamefikisha alama 12 kwa mechi nne walizocheza na kuendelea kushika usukani wa msimamo wa Ligi Kuu Vodacom.

Matokeo ya mechi nyingine uwanja wa Kaitaba Mjini Bukoba Kagera Sugar wameendelea kugawa pointi baada ya kuchapwa tena 1-0 na JKT Tanzania.

Mtibwa Sugar wamebanwa mbavu na Mbeya City ya kufungana 1-1,Lipil FC 2-2 dhidi Tanzania Prisons na KMC wamelazimishwa sare ya 1-1 na Ndanda FC uwanja wa Chamazi nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam