Meneja wa Mauzo na Biashara wa TBL Afrika mashariki Bi.Edith Bebwa,akiongea wakatiwa mahafali hayo.
………………
Kampuni ya Bia Tanzania chini ya kampuni ya kimataifa ya ABInBEV, Mwishoni mwa wiki iliwatunuku vyetiwahitimu waMafunzo ya kukuza Biashara kwa wajasiriamali wadogo yaliyoendeshwa katika mikoa ya Dar es Salaan na Dodoma.
Haya ni mahafali ya pili tangu kuanzishwa kwa programu hii ya kukuza biashara kwa wajasiriamali wadodo hapa Tanzania mwaka Jana, 2018.
Akizungumza katika hafla hiyo, Meneja wa Mauzo na Biashara wa TBL Afrika Mashariki Bi.Edith Bebwa alisema, “Programu hii ambayo inajulikana zaidi kama RDP, imefanikiwa kuwafikia washiriki 183 ikiwa ni ongezeko la 11% ukulinganisha na mwaka jana. Wengi wa washiriki ni wamiliki na wasimamizi wa baa mbalimbali kutoka katika mikoa hii miwili ya Dar es salaam na Dodoma.
“Leo tarehe 26 Septemba 2019, tunayo furaha kuwatunuku vyeti wajasiriamali hawa wa Dar es salaam waliopata mafunzo kwenye wilayani zao yaani Temeke (iliyojumuisha Temeke na Kigamboni),Kinondoni,Ubungo na Ilala.Washiriki hawa wamepatiwa mafunzo yaliyoandaliwa na kufundishwa kitalaam ili yaweze kusaidia kuendelezana kukuza biashara zao na hatimaye kuchangia zaidi uchumi wa taifa kupitia kodi na ajira. Mafunzo haya yalitolewa katika namna mbili, moja mafunzo ya nadharia darasani na pili mafunzo na ushauri katika maeneo yao ya biashara”. Alisema Bebwa.