********************************
Msanii nyota Afrika Mashariki na ya Kati wa nyimbo za injili Christina Shusho ameandaa kongamano la kimataifa jijini Dar es salaam, ambao anatarajia kuleta nguvu mpya kwa Tanzania na mataifa mengine ambayo yatawakilishwa kwenye mkutano huo.
Kongamano hilo “Eagles Meet International Conference-EMIC)” la siku sita, kuanzia tarehe 1 Novemba 2019, litakuwa na wahamasishaji wa kimataifa pamoja na wanamuziki mashuhuri.
Pamoja na kuwa shukurani kwa Mungu, Kongamano litajadiliana kile ambacho watu, mataifa, wanaweza kufikia ikiwa watamuogopa Mungu, huku wakikaa katika upendo na kufanya kazi kwa bidii.
“Hapa Tanzania, tumeona maendeleo makubwa yanafanyika. Katika ulimwengu wa kiroho, watu wanahitaji kutazama haya na kumshukuru Mungu. Lakini pia tunastahili kuomba hekima, ili kila mmoja aweze kuchukua hatua, kufanya anayostahili, kwa njia sahihi, na wakati unaofaa. Hii kwa ajili ya maendeleo ya taifa letu na kwa maendeleo ya mtu binafsi, ” alibaini Madam Shusho, ambaye pia ni Rais na Mwanzilishi wa Kituo cha Dreamers Center Tanzania.
Akizungumza katika mahojiano Shusho alisema ombi lake kwa kila Mtanzania, kumtumaini Mungu na kuanza kuwa na ndoto kubwa.
Shusho anasema kwamba maono makubwa ni muhimu sana kutoka ngazi ya mtu binafsi, familia na taifa kwani yanafungua baraka.
Nina ndoto kubwa kwa nchi yangu, kwa ajili yangu na kwa kanisa, alisema.
“Rais wetu Dk John Magufuli ametuonyesha njia. Angalia miradi mikubwa ya miundombinu katika nchi yetu ambayo tulikuwa hatujawahi kuiona. Lazima tuache kuhisi sisi ni wadogo, ni watu wa chini- tuwe na ndoto kubwa, tuwe na maono makubwa. Ninazungumza juu ya kila mtu, watoto, watu wazima, viongozi na wote,” alisema.
Shusho, ni nyota wa nyimbo za injili ambazo huchezwa kote Afrika Mashariki na Kati, ambapo Kiswahili kinatumika, naye pia bali na kuratibu kongamano, atakuwa mmoja wa wasemaji wakuu.
Baadhi ya watu mashuhuri watakao zungumza kwenye hafla hiyo ni pamoja na Dk Jeremiah Kapotwe (kutoka Afrika Kusini), ambaye ni mwandishi wa kitabu kinaitwa Ufanye Nini Shida Inakapokuja (What Do You Do When Trouble Comes) na Apostle Stephen Kato (kutoka Uganda), mwandishi wa Kitabu kinaitwa Mtu wa Hatima “Man of Destiny.”
Kutoka Kenya, anakuja Askofu Chris Mwashumbe mwanzilishi wa Kituo cha River Of Life Centre.
Tanzania itawakilishwa na wahamashishaji mashuhuri kama Mwalimu Teddy Kwilasa, Askofu Mulenda Omary, Rev Joseph Mayala na wengine.