Wachezaji Kutoka kulia Merci Nyanchama wa Kenya Peace Kabasweka wa pili kulia wakibadilishana matokeo na Angel Eaton wakwanza Kushoto na Hawa Wanyenche wa Pili Kushoto wote wa Lugalo mara baada ya kumaliza mchezo kwa Siku ya pili ya mashindano ya wazi ya Wanawake Tanzania katika Uwanja wa TPC Moshi (Picha na Luteni Selemani Semunyu).
Wachezaji Merci Nyanchama wa Kenya na Peace Kabasweka kulia na Angel Eaton na Hawa Wanyenche kushoto wa Lugalo wakipongezana mara baada ya kumaliza mchezo kwa Siku ya pili ya mashindano ya wazi ya Wanawake Tanzania katika Uwanja wa TPC Moshi (Picha na Luteni Selemani Semunyu).
********************************
Na Luteni Selemani Semunyu
Mashindano ya golf ya wanawake Tanzania yamefikia siku ya pili huku wachezaji kutoka klabu ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania ya Lugalo wakichuana vikali na mchezaji kutoka Uganda Peace Kabasweka.
Mchezaji huyo wa Uganda aliongoza tangu siku ya kwanza kwa fimbo mbili dhidi ya Angel Eaton wa Lugalo akifuatiwa na Hawa Wanchenche wa Lugalo pia.
Licha ya kuongoza kwa fimbo mbioli siku ya kwanza mchezaji huyo kutoka uganda alisema bado mchezo ni mgumu na matumaini ya kuibuka na ushindi bado ni magumu na mwamuzi ni siku ya mwisho ya mchezo
“ Wachezaji kutoka Lugalo ni Wakali na Wanajituma na Idadi ya Fimbo ninazoongoza ni chache hivyo ukifanya mzaha kidogo basi ni rahisi kufungwa hivyo bado naweza kusema Mchezo ni Mgumu” Alisema Kabasweka
Naye Mchezaji kutoka Lugalo Angel Eaton aliyekuwa akimfuatia alisema peace ni Mchezaji mzuri na mchezo bado uko upande wake lakini hakuna kukata tamaa mpaka dakika ya mwisho.
“ Nimetumwa na klabu yangu ushindi hivyo nitapambana kuhakikisha ubingwa unakwenda lugalo mengine tumwachie mungu kwani kuna wachezaji wazuri tu na wanacheza vizuri mpaka sasa “ Alisema Angel.
Kwa Upande wake mchezaji Hawa Wanchenche naye kutoka kutoka klabu ya Lugalo alisema wamepangwa kundi moja leo kutokana na mchezao mzuri na hapa tunawania ubingwa lakini pia nafasi kushiriki mashindano nchini Uganda.
Kutoka Kenya ambao nao wameshiriki katika mashindano haya mchezaji Merci Nyanchama kutoka kwa upande wake alisema amecheza vibaya hivyo hana matumaini ya ushindi lakini kiujumla mashindano ni mazuri na yamevutia.