Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Atashasta Nditiye (wa kwanza
kushoto)akikabidhi kitabu chenye orodha ya minara iliyojengwa na Mfuko wa
Mawasiliano kwa Wote kwa Katibu Tawala wa Wilaya ya Kibondo, Ayubu Sebabili, akiwa ziarani Kigoma. Anayeshuhudia wa kwanza kulia ni Justina Mashiba, Kaimu Mtendaji Mkuu wa Mfuko huo.
Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Atashasta Nditiye (wa kwanza kulia) akimsikiliza kwa makini Justina Mashiba (wa kwanza kushoto), Kaimu Mtendaji Mkuu wa Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote, akitoa maelezo kuhusu mnara wa Itaba wakati wa ziara yake ya kukagua upatikanaji wa huduma za mawasiliano, Kigoma.
Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Atashasta Nditiye (wa kwanza kulia) akitoa maelekezo kwa Kaimu Mtendaji Mkuu wa Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote, Justina Mashiba ((wa kwanza kushoto) ya kuhakikisha kuwa mnara wa Itaba, unawaka muda wote ili wananchi wapate mawasiliano, akiwa ziarani Kigoma.
Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Atashasta Nditiye
(aliyesimama)akihamasisha wananchi wa Kijiji cha Kigina kusajili laini za simu zao za mkononi wakati wa ziara yake mkoani Kigoma ya kukagua upatikanaji wa huduma za mawasiliano.
Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Atashasta Nditiye (anayetembea mbele) akitoka kukagua mnara wa Itaba akiwa katika ziara yake ya kukagua upatikanaji wa mawasiliano mkoani Kigoma.
****************************
Na Prisca Ulomi, Kigoma.
Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye amesema kuwa mwananchi hataweza kupiga wala kupigiwa simu kama hajasajili laini ya simu yake ya mkononi kwa alama za vidole ifikapo tarehe 31 Desemba, 2019.
Nditiye ameyasema hayo akiwa kwenye ziara yake ya kikazi Mkoani Kigoma kwenye wakati akihamasisha na kuelimisha wananchi wa Kata ya Ruhita, Kibuye, Mrufiti, Itaba, Murungu, Rugongwe, Kasulu na Kibondo mjini umuhimu wa kusajili laini zao za simu za mkononi.
“Serikali imeamua watanzania wote wasajili laini zao za simu za mkononi kwa kutumia alama za vidole ili kila anayepiga simu au kupigiwa atambulike ili kupunguza changamoto zinazojitokeza ili mawasiliano yaweze kuchangia kikamilifu uchumi wa chi yetu,” amesema Nditiye.
Amefafanua kuwa Sekta ya Mawasiliano imeshika nafasi ya tatu kwa mwaka 2016/2017 na ya nne kwa mwaka 2017/18 kwa kuchangia pato la taifa kwa kiwango cha asilimia 13.1 na kuwa kati ya Sekta tano bora zinazochangia pato la taifa. Serikali ieamua kusimamia kikamiifu Sekta hii ili kuhakikisha kuwa inadhibiti wizi wa mtandaoni kupitia simu za mkononi, ulaghai, uchochezi, utapeli a matumizi mengine ya simu za mkononi kwa kuwa kila mwanachi atakuwa amesajili laini yake ya simu ya mkononi kwa alama ya kidole.
Amewahamasisha wananchi waishio maeneo mbali mbali mkoani humo wakati
alipofanya nao mkutano wa hadhara kuwa kuanzia mwezi Oktoba mwaka huu,
wataalamu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania wakiambatana na kampuni za simu za mkononi, Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa, Jeshi la Polisi na Uhamiaji watafika maeneo mbali mbali mkoani humo ili kuendesha zoezi la kusajili laini za simu kwa wananchi wote wanaotumia na kumiliki simu za mkononi.
Amesema kuwa zoezi hili litafanyika kwa umakini mkubwa ili kuhakikisha kuwa
watanzania halali wanaotambulika na wenye kadi ya NIDA au namba ya utambulisho kutoka NIDA wanasajili laii zao ili kuepusha kufanya usajili kwa watu wasiohusika kwa kuwa mkoa wa Kigoma uko mpakani ambapo kuna mwingiliano wa watu kutoka nchi za jirani.
Naye Japhet Amos, mkazi wa kijiji cha Kigina kilichopo kata ya Rugongwe, Kigoma akizungumza kwa niaba ya wananchi wenzake alimuomba Nditiye kuhakikisha kuwa wananchi wanapata kitambulisho cha NIDA au namba ya utambulisho kwa wakati ili wasizimiwe simu zao mara baada ya tarehe ya wisho iliyowekwa na Serikali kufika a kuomba huduma hiyo ya usajili itolewe bure.
Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania, Kanda ya Kati, Antonio Manyanda
aliwafahamisha na kuwatoa hofu wananchi wote nchi nzima kuwa huduma ya kusajili laini ya simu ya mkononi kwa alama ya kidole ni bure na hakuna mwananchi yeyote atakayelazimika kulipia gharama hiyo na ametoa wito kwa wananchi kuiarifu TCRA yenye ofisi zake sehemu mbali mbali nchini kuhusu jambo hilo endapo mwananchi yeyote atatozwa gharama za kusajili laini yake na wakala wa kampui yeyote ya simu.
“Usajili wa laini ya simu kwa alama ya vidole ni bure nchi nzima, mwananchi haruhusiwi
kulipa gharama yeyote kwa ajili ya kusajili laini ya simu,” amesisitiza Manyanda.
Katika hatua nyingine, akiwa ziarani mkoani humo, Nditiye amekagua upatikanaji wa
mawasiliano kwenye kata ya Kibuye, Murungu, Rugongwe na Itaba na kutembelea
minara inayotoa mawasiliano kwa wananchi waishio maeneo hayo na kubaini uwepo
wa mawasiliano wakati wa asubuhi na jioni na kufifia au kukosekana kabisa wakati wa
usiku ambapo ameiagiza UCSAF kwa kushirikiaa na TCRA na kampuni za simu zenye
minara yake maeneo hayo kuongeza betri za kutosha ili kuapata umeme wa jua wa
kuendesha minara hiyo kwa lengo la kuwawezesha wananchi kupata huduma za
mawasiliano hata nyakati za usiku.
“Mawasiliano yako chini sana, mtu anapatikana kuanzia saa tatu asubuhi hadi saa kumi
na moja jioni, matukio yanatokea usiku hatuna msaada na tuna mtandao mmoja tu wa
Vodacom,” amesema Emil Mfanye, Diwani wa Kata ya Murungu akizungumza kwa
niaba ya wananchi kwenye mkutano wa hadhara wa Nditiye na wakazi wa kijiji cha
Kumhasha alipokuwa kwenye ziara yake mkoani humo ya kukagua upatikanaji wa
huduma za mawasiliano, kuhamasisha wananchi kusajili laini za simu kwa alama ya
vidole na kutoa elimu ya manufaa ya anwani za makazi na postikodi