Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Balozi Seif Ali Idd (katikati) akiwasili katika Tamasha la maonesho ya utamaduni wa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki kwa ajili ya kufunga tamasha hilo lilofanyika kwa siku nane katika uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, kulia ni Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe.
Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Balozi Seif Ali Idd akifurahia jambo na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe (katikati) na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Dk. Aloyce Nzuki wakati Makamu wa Rais alipotembelea banda la
wizara hiyo kwa ajili ya kufunga Tamasha la maonesho ya utamaduni wa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki lilofanyika kwa siku nane katika uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Balozi Seif Ali Idd akiangalia picha mbalimbali za kumbukumbu katika banda la Maliasili na Utalii kabla ya kufunga Tamasha la maonesho ya utamaduni wa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki lilofanyika kwa siku nane katika uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Balozi Seif Ali Idd akimkabidhi cheti Mwenyekiti wa Kitaifa wa Kamati ya Tamasha la Utamaduni wa nchi za Afrika Mashariki wakati wa kufunga tamasha hilo lilofanyika kwa siku nane katika uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Balozi Seif Ali Idd akimkabidhi cheti Kaimu Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania Dkt. Kiagho Kilonzo wakati wa kufunga Tamasha la Utamaduni wa nchi za Afrika Mashariki lilofanyika kwa siku nane katika uwanja wa Taifa jijini Dar es
Salaam.
Msanii Mrisho Mpoto (mwenye nguo nyeusi) akitoa burudani na kikundi chake wakati wa kufunga Tamasha la maonesho ya utamaduni wa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki lilofanyika kwa siku nane katika uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Balozi Seif Ali Idd akisisitiza jambo kwa washiriki wa Tamasha la Utamaduni wa nchi za Afrika Mashariki kabla ya kulifunga tamasha hilo hii leo katika uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Picha na WHUSM –Dar es Salaam