Home Mchanganyiko RC MAHMOUD AMESEMA ATAENDELEA KUSHIRIKIANA NA WANANCHI KATIKA KUTATUA CHANGAMOTO WANAZOZIPATA

RC MAHMOUD AMESEMA ATAENDELEA KUSHIRIKIANA NA WANANCHI KATIKA KUTATUA CHANGAMOTO WANAZOZIPATA

0

Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Hassan Khatib Hassan wa (Kati Kati ) akimkabidhi hati za Ofisi Mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja Ayoub Mohamed Mahmoud wa kwanza ( Kulia) huko Ofisini kwake Tunguu.

Mkuu wa Wilaya ya Kati Unguja Hamida Mussa Khamis akimkabidhi zawadi ya Picha Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Hassan Khatib Hassan wa (Kati Kati ) huko Ofisini kwake Tunguu.

……………………

Na Mwashungi Tahir,Maelezo

Mkuu wa Mkoa ya Kusini Unguja Ayoub Mohamed Mahmoud amesema ataendelea   kushirikiana na wananchi katika kusikiliza shida zao  na kukaa kwa pamoja ili kuzipatia ufumbuzi.

Ameyasema  hayo katika Hafla ya makabidhiano ya hati ya Ofisi  yaliyofanyika katika Ukumbi wa Mkoa wa Kusini  ulioko Tunguu na kuwataka wafanyakazi wajenge mashirikiano katika utendaji wa kazi na kuweza kupata maendeleo.

Amesema katika Mkoa  wa Kusini atahakikisha Mkoa unakuwa upo katika hali ya amani na usalama akiwa kama ni kiongozi alokabidhiwa jukumu atalisimamia vizuri na kulifanyia kazi .

Pia amesema anamshukuru Rais wa Zanzibar kwa kuwaamini na kuwapa nafasi hizo hivyo anaahidi kwa moyo wa dhati katika kutekeleza Ilani ya Chama cha Mapinduzi na kuhakikisha Mkoa huo unashinda ushindi wa kishindo ifikapo 2020.

Aidha ameeleza kuwa ataendelea kutumia vyombo vya habari ili kuijuilisha jamii kila kinachotokea kwani hiyo ndio sera ya habari na mawasiliano.

“Nitahakikisha naendelea kutumia wanahabari katika kuwapa taarifa jamii kwa kila linalotokea ili waweze kutambua maendeleo na  kufaidika”, alisema Ayoub.

Nae Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Hassan Khatib  Hassan Alisema Katika Mkoa wa Kusini mambo mengi yamekuwa yako vizuri ikiwemo amani na utulivu kwa kushirikiyana na vyombo vya ulinzi na usalama.

Pia ameeleza kwamba kwa kiasi kikubwa ukusanyaji wa mapato umekuwa wa kuridhisha na kuhusu mogogoro ya ardhi ilikuwa ikisumbua lakini kwa hivi sasa imepungua.

Hivyo amewataka wafanyakazi wa mkoa huo kumpa mashirikiyano ili aweze kutekeleza majukumu ya katiba na sheria katika utendaji wa kazi.

Na kwa upande wa Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Wilaya ya Kati Hassan Mrisho Vuai amemshukuru Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi wakati alipokuwa katika Mkoa wa Kusini kwa kushughulikia mambo mengi ya maendeleo ikiwemo kuimariha vikundi vya ushirika.