Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) akikagua shamba la mfano la kahawa wakati alipotembelea kwenye Taasisi ya utafiti wa kahawa Tanzania (TaCRI) Mkoani Songwe tarehe 26 Septemba 2019. (Picha Zote Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo)
Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) akisaini kitabu cha wageni tarehe 26 Septemba 2019 mara baada ya kutembelea Taasisi ya utafiti wa kahawa Tanzania (TaCRI) Mkoani Songwe, Mwingine pichani ni Mwenyekiti wa Taasisi ya utafiti wa kahawa Tanzania (TaCRI) Ndg Aloyce Mdalavuma (Kulia).
Meneja wa kituo cha utafiti wa Kahawa Mkoani Songwe Ndg Isack Mushi akimuelezea Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) kuhusu kilimo bora cha kahawa wakati akikagua shamba la mfano la kahawa alipotembelea kwenye Taasisi ya utafiti wa kahawa Tanzania (TaCRI) Mkoani Songwe tarehe 26 Septemba 2019.
Na
Mathias Canal, Wizara ya Kilimo-Songwe
Mathias Canal, Wizara ya Kilimo-Songwe
Serikali imepanga kubadilisha kilimo kutoka kuwa
cha kujikimu na kuwa kilimo cha kibiashara kama ilivyoainishwa katika Dira ya
Taifa ya Maendeleo 2025 kwa kuzingatia mazao ya kipaumbele.

Miongoni mwa mazao hayo ya kipaumbele ni kahawa
ambapo katika mwaka wa fedha wa 2019/2020, Wizara ya Kilimo kupitia Bodi ya
Kahawa imepanga kuongeza uzalishaji kutoka tani 65,000 hadi tani 80,000. Aidha
bodi imepanga kuzalisha na kusambaza miche milioni 10 ya kahawa katika
wilaya 42.

Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb)
ameyasema hayo leo tarehe 26 Septemba 2019 wakati akizungumza na watendaji wa Taasisi
ya utafiti wa kahawa Tanzania (TaCRI) alipotembelea taasisi hiyo Mkoani Songwe.

Alisema kuwa zao hilo lina mchango mkubwa kwa
uchumi wa Taifa na kwa maendeleo ya jamii lakini katika miaka ya karibuni
lilionekana kuzorota kutokana na kuwapo kwa changamoto mbalimbali.

Kutokana na hali hiyo Serikali imeendelea kubuni
mikakati mipya ya taratibu za usimamizi wa sekta hiyo ili kuleta ufanisi katika
uzalishaji wa zao hilo.

Mhe Hasunga amesema kuwa ili kuongeza uzalishaji
wenye tija katika zao la kahawa serikali imejipanga kuimarisha upatikanaji wa
miche bora kwa ajili ya kuzisambaza kwa wakulima nchini.

Pia ameipongeza Taasisi hiyo kwa kutoa elimu kwa
wakulima kuhusu matumizi sahihi ya mbegu bora za kahawa huku akisisitiza
taasisi hiyo kuongeza weledi katika utoaji elimu kwa wakulima.

Naye, Mwenyekiti wa Taasisi ya utafiti wa
kahawa Tanzania (TaCRI) Ndg Aloyce Mdalavuma ameiomba wizara ya Kilimo kwa
ushrikiano na wataalamu mbalimbali wa TaCRI kuongeza juhudi ili kuongeza tija
na uzalishaji wa kahawa.

Pia amesema kuwa uwezo wa Taasisi hiyo katika kuzalisha
mbegu bora bado ni mdogo hivyo ameiomba serikali kuongeza uwezekano ili
kuzalisha mbegu nyingi ambazo zitawafikia wakulima wengi.

Kwa upande wake Meneja wa kituo cha utafiti wa
Kahawa Mkoani Songwe Ndg Isack Mushi ameeleza kuwa jukumu kuu la TaCRI ni
kurudisha matumaini ya tasnia ya kahawa kwa kutoa na kusambaza teknolojia za
kuendeleza zao la kahawa kwa ajili ya kuongeza tija katika uzalishaji na ubora.

Nyingine ni kupunguza gharama za uzalishaji,
kuboresha kipato na riziki kwa wakulima wote wa kahawa na kuongeza mchango wa sekta
ya kahawa kwenye pato la Taifa.