Naibu Waziri wa Afya Harusi Said Suleiman akisisitiza jambo alipotoa hotuba katika maadhimisho ya siku ya Wafamasia Duniani yaliofanyika Viwanja vya Mnara wa Kumbukumbu ya Miaka 50 ya Mapinduzi Kisonge Zanzibar.Ujumbe wa mwaka huu ni Usalama na ufanisi wa Dawa kwa wote.Wafamasia kutoka katika Vituo mbalimbali wakiwa katika Maandamano kuadhimisha siku ya Wafamasia Duniani yaliofanyika Viwanja vya Mnara wa Kumbukumbu ya Miaka 50 ya Mapinduzi Kisonge Zanzibar.Ujumbe wa mwaka huu ni Usalama na ufanisi wa Dawa kwa wote.
Naibu Waziri wa Afya Harusi Said Suleiman (wapili kushoto)akipokea maandamano ya Wafamasia kuadhimisha siku ya Wafamasia Duniani yaliofanyika Viwanja vya Mnara wa Kumbukumbu ya Miaka 50 ya Mapinduzi Kisonge Zanzibar.Ujumbe wa mwaka huu ni Usalama na ufanisi wa Dawa kwa wote.
-Naibu Waziri wa Afya Harusi Said Suleiman akionesha kitabu cha (ANATOMIA NA FIZIOLOJIA) kinachoelezea somo la Maumbile ya Binaadam na Ufanyaji kazi kilichotungwa na Mfamasia Hassan Zubeir ambacho amekizindua katika maadhimisho ya siku ya Wafamasia Duniani yaliofanyika Viwanja vya Mnara wa Kumbukumbu ya Miaka 50 ya Mapinduzi Kisonge Zanzibar.Ujumbe wa mwaka huu ni Usalama na ufanisi wa Dawa kwa wote.
PICHA NA YUSSUF SIMAI/MAELEZO ZANZIBAR.
*******************************
Na Maryam Kidiko – Maelezo Zanzibar. 26/09/2019.
Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar itaendelea kutilia mkazo suala la afya za wananchi kwa kuwapatia dawa bora na sahihi ili kuimarisha hali zao za afya.
Hayo aliyasema Naibu Waziri wa Afya Harusi Said Sleiman Mnara wa Kumbu kumbu Kisonge kwenye maadhimisho ya siku ya Wafamasia Duniani.
Amesema kuwa Wafamasia wanajukumu kubwa la kuhakikisha wanatumia taaluma yao ili kuwasaidia wagojwa na kuonekana afya zao zinaimarika.
Amewataka kutumia kauli nzuri na kuwaelekeza Wagojwa matumizi sahihi ya dawa ili kulinda afya zao na kuepusha matatizo yasioyo ya lazima.
“Nijukumu lenu Wafamasia kulinda afya za Wagojwa na muwe na kauli nzuri kwao mnapowaelekeza juu ya matumizi ya dawa ili kuepuka athari za matumizi mabaya ya dawa,” alisema Naibu Waziri wa Afya.
Hata hivyo aliwataka Wafamasia kutoa mafunzo kwa jamii iliyowazunguka juu ya matumizi ya dawa ili kuacha tabia ya kutumia dawa bila kupata maelekezo kutoka kwa daktari.
Kaimu Mfamasia Mkuu wa Wizara ya Afya Zaharani Ali Hamadi aliahidi watahakikisha kuwa wanatimiza lengo lililokusudiwa la kuwapa maelekezo mazuri Wagojwa wanapopatiwa dawa.
Alisema Taifa kuwa na afya bora linahitaji maelekezo na miongozo mizuri hivyo watatumia taaluma yao kuhakikisha wanawasaidia wananchi.
Zahran alieleza kuwa Wafamasia duniani kote wamekua wakiadhimisha siku hiyo kila mwaka na kwa Zanzibar hii ni mara ya kwanza na wataendelea kuadhimisha siku hiyo kila ifikapo taehe 25 Septemba.
Akitoa Elimu ya matumizi sahihi ya dawa, mfamasia Bora Lichanda alisema mtu anapoumwa lazima amuone Daktari na kuacha kutumia dawa bila ya maelekezo.
Amewashauri Wananchi wanapopata matatizo ya kuumwa kuacha kutumia dawa zilizobakishwa na mgonjwa mwengine kwani kufanya hivyo ni kuhatarisha afya zao.
“Ninawaomba kuacha kutumia dawa za mgonjwa mwengine ama zilizokaa kwa mda mrefu kwani kufanya hivyo ni kuhatarisha afya zenu, ”alisema Mfamasia Lichanda.
Kila ifikapo tarehe 25 Septemba ni siku ya Wafamasia duniani ambapo kauli mbiu ya mwaka huu ni “Usalama na ufanisi wa Dawa kwa wote “ kauli mbiu ambayo ina lengo la umuhimu wa Mfamasia kulinda hali ya Mgojwa.