Nimeiona taarifa kutoka klabu ya Yanga, ikizungumzia juu ya uteuzi wa kamati ya ufundi na nilipoisoma nikakuta imesheheni majina ya vigogo waliobobea katika medani za ufundi wa soka hapa nchini hususani klabu hiyo ya Yanga
Mara likanijia swali muhimu sana, nini jukumu la kamati hiyo? Swali hili lilinijia kwa kuwa mimi si muumini sana wa hizi kamati (ingawa si kosa)
Tatizo langu kwa kamati hizi ni majukumu na wajibu wake, sijawahi kuona zikiwa nguvu ninazotamani wawe nazo.
Najaribu kuwaza kamati hii ingekuwa ndiyo iliyowasajili Kalengo na Bigirimana, pia ingekuwa ndiyo kamati inayoshughulikia madai na mkataba wa “Dante”, au kamati kama hii ingekuhusika na mauzo ya Makambo au wao ndo wangetuambia Molinga yupo kwa mkopo au la, na kama nu mkopo je? Kuna kipengele cha kumnunua moja kwa moja?
Endapo kamati hii ingehusika kikamilifu kupanga kambi ya Yanga kule Arusha kabla ya mchezo wa marudiano dhidi ya Rollers, lakini pia kamati hii ingekuwa ndiyo iliyoingia mkataba na Mwinyi Zahera na wakampa mahitaji ya mkataba huo.
Meno haya sijuwi kama ndo yanaanza kuota au kamati hii ni kama hadithi ya ndama wa ng’ombe na meno ya juu.
Kamati sawa, lkn meno yako wapi?