***************************************
Na Hamoud Abdallah
Nianze kwa kuucheza mpira nje ya uwanja. Ivi unajiskiaje kumuona mwenzako ambaye umesoma naye, akiwa na maendeleo kukuzidi we we?
Tena wakati mwingine inawezekana na darasani alikuwa anajificha kwenye kivuli chako, ukiwa ulikua unamsaidia kwenye maswala ya kitaaluma au mpaka kumpa majibu kwenye mitiani. Na endapo isingekua wewe basi historia nyingine ingejiandika.
Haikuishia hapo kutokana na nafasi ya wanao kusimamia, wakaona uondoke pale ulipokuwa na swaiba yako uende mahala pengine ambapo utafanya vyema zaidi.
Lakini kama maisha yalivyo tabiriwa kuwa ni Safari na hatujui litakalo tokea kesho, kumbe Yale maamuzi ya kuhamishwa/kuhama pale ulipo naweza sema ni sawa na uliruka haja ndogo na ukakanyaga haja kubwa. Yaani ni bora ungesalia pale ulipo pengine ungekua na mafanikio kama ya swahiba yako ama zaidi yake.
Kipenga kikiwa kimelia na nimekwisha pasha misuli tayari kwa kipute, ni muda sasa wa kuucheza mpira ndani ya uwanja.
Rhian Joel Brewster ni mchezaji wa kimataifa wa Uingereza, anayekipiga ktk club ya Liverpool huku piya akiwa analiwakilisha taifa lake kuanzia ngazi za chini mpaka sasa akiwa kwenye timu ya U20.
Maisha yake ya soka aliyaanza akiwa kwenye Academy ya Chadwell Health and Shield akiwa na umri chini ya miaka saba. Alipofikisha umri wa miaka saba alifanikiwa kujiunga na club ya Chelsea akiwa katika mikono ya kocha Michael Beale mpaka pale alipofikisha umri wa miaka 14 na baadaye aliamua kubadilisha hali ya upepo alipotimka darajani na kujiunga na majogoo wa jiji La Liverpool.
Mafanikio yake ndani ya Liverpool yanajieleza, kwani ameshafanya vizuri kwenye timu ya vijana ikapelekea kuwa miongoni mwa wachezaji walioliwakilisha taifa lake la Uingereza kwenye michuano ya kombe La Dunia la vijana wenye umri chini ya miaka 18 (mwaka 2017) huku wakitwaa taji hilo na kubwa zaidi akiibuka mfungaji bora na kushinda tuzo ya kiatu cha dhahabu kwenye michuano hiyo.
Ndani ya club tayari anaye medali kadhaa ikiwemo ile ya ubingwa wa UEFA champ, na Super Cup lakini ni medali ambazo zimeingia kwenye CV yake bila ya kuhusika yaani hajazitolea jasho uwanjani jambo ambalo anatamani iwe ivyo.
Mwaka 2014 wakati Brewster anajiunga Liverpool akitokea Chelsea, sababu iliyopelekea kufanya maamuzi hayo ni baada ya kuamini kuwa pale anfield ni njia rahisi ya kucheza kwenye timu ya wakubwa kuliko aliko toka, baada ya kuona vijana kama kina Sterling, Flanagan na hivi karibuni kina Joe Gomez, Alexander Arnold wanapewa nafasi.
Licha ya kuwa kwenye mipango ya kikosi cha kwanza cha Klopp hasa baada ya kocha huyo kuwaruhusu kina Solanke, Ings na Sturedge kuondoka bila ya kuziba nafasi zao huku akiwa na washambiliaji wawili pekee kwenye eneo la kati yaani Firmino na Origi, bado hatujamuona Brewster yule ambaye wengi wanamtegemea.
Pengine Brewster hajaruka haja ndogo na kukanyaka haja kubwa kutokana na Umri wake bado unaruhusu (19), lakini tukirudi nyuma kipindi kile yupo kwenye academy ya Chelsea na kina Fikayo Tomori, Mason Mount, Callum Hudson-Odoi na Tammy Abraham (maswaiba) akaamua kuwakimbia na kuelekea Liverpool akiamini atapata nafasi kwenye timu ya wakubwa, tayari wenzake wameshampiku na ni wachezaji wa kikosi cha kwanza.
Msimu ulioisha alionesha dhamira ya kugomea kuongeza mkataba baada ya kuona nafasi yake ni finyu kutinga kwenye timu ya wakubwa huku vilabu kutoka Ujerumani na Italia vikionesha nia ya kumtaka. Naweza kusema endapo asingepata majerui yaliyemuweka nje kwa takribani msimu mzima Leo hii Brewster asingekua Mali ya Liverpool.
Maneno mazuri ya Klopp yalimfanya kinda huyo aweze kubadilisha maamuzi yake na kuongeza kandarasi nyingine ya muda mrefu. Ni ngumu kwa Brewster kubomoa ule utatu pale mbele, lakini kwa uwezo aliounesha kwenye michezo ya Preseason kilichobakia ni Klopp kumng’arisha kwa kuanza kumsindikiza taratibu kwenye kikosi cha kwanza ili kumjenga kisaikolojia asione kuwa alikosea kujiunga na Liverpool kutokana na wenzake wanavyofanya vizuri na ikapelekea kuingia kwa mtetereko kwenye soka lake, ama ikapelekea kulazimishwa kuuzwa na timu ikakosa huduma yake.
Mtanange wa EFL cup dhidi ya Milton Keynes Dons upo mbele yake na nadhani utakua muda sahihi kwa Klopp kuanza kumpa nafasi pamoja na makinda wengine akiwemo mlinda lango Caoimhin Kelleher, Curtis Jones na Harvey Elliott.