Wafanyakazi wa TBL Ilala, wakiwa katika hafla ya kukabidhi taulo za kike kwa mwakilishi wa taasisi ya Her Africa.
Meneja wa TBL kiwanda cha bia cha Ilala jijini Dar es Salaam Calvin Martin, akiongea wakati wa hafla ya kukabidhi msaada wa taulo za kike 1,600 zilizochangwa na wafanyakaz
Meneja wa Masuala Endelevu wa TBL, Irene Mutiganzi akiongea wakati wa hafla hiyo.
Mwanzilishi wa taasisi ya Her Africa Asnath Ndosi,akitoa neno la shukrani wakati wa hafla hiyo.
………………..
Wafanyakazi wa kampuni ya Tanzania Breweries Limited- (TBL), chini ya kampuni mama ya ABInBEV kutoka viwanda vilivyopo katika mikoa ya Dar es Salaam, Mwanza,Arusha na Mbeya, wametoa msaada wa taulo za kike za kuwakinga wasichana wakati wa vipindi vya hedhi wawapo mashuleni kwa taasisi ya Her Africa kupitia kampeni yake ijulikanayo kama “Hedhi yangu Furaha Yangu”
Akiongea wakati wa kukabidhi msaada huo,Meneja wa Kiwanda cha TBL cha Ilala jijini Dar es Salaam,Calvin Martin,alisema wafanyakazi wa kampuni wameguswa na changamoto hiyo inayowakabili wasichana wengi hasa wanaotoka kwenye familia za kawaida na kuamua kujitoa kukabiliana nayo katika viwanda vyote na aliwashukuru kwa moyo wao wa kujitoa.