Home Mchanganyiko MKUU WA WILAYA YA MALINYI KUANZA KAZI RASMI

MKUU WA WILAYA YA MALINYI KUANZA KAZI RASMI

0

 NA FARIDA SAIDY ,MOROGORO

MKUU wa wilaya ya Malinyi Bw. Mathayo Masele  amesema anafahamu changamoto mbalimbali zilizopo katika wilaya hiyo ikiwemo  Afya na Elimu hivyo atajitahidi kushirikiana na watendaji wa serikali na wananchi ili kuzitatua changamoto hizo

Mkuu wa wilaya huyo ameyasema hayo  mara baada ya kula kiapo cha utumishi  katika ofisi ya mkuu wa mkoa wa Morogoro ambapo amesema   Rais Magufuli amemuami ndomana amemteua hivyo atahakikisha  anajitahidi kutauatua changamoto zinzowakabili wananachi wa wilaya hiyo.

Kwa upande wake mkuu wa mkoa wa Morogoro  Loata Ole Sanare amemtaka mkuu huyo wa wilaya kusimamia kikamiligu fedha za miradi ya serikali inayotekelezwa na seruikali wilayani hapo huku katibu tawala mkoa Huo mhandisi Emanuel Kalobero amesema  lengo la Rais Magufuli ni kuwaletea manedeleo wananachi hivyo viongozi ambao wameaminiwa wanatakiwa kufanya kazi kwa uaminifu na kuzingatia maadili ya uongozi

Aidha Bi. Regina Chonjo  ni mkuu wa wilaya ya Morogoro amemshauri mkuu huyo mpya wa Wilaya ya Malinyi kuangalia dira ya viongozi wakubwa wa kitaifa  katika utendaji wa kazi.