Home Mchanganyiko WADAU WA ELIMU WAKUTANA KUFANYA TATHMINI YA UTEKELEZAJI MALENGO YA MWAKA

WADAU WA ELIMU WAKUTANA KUFANYA TATHMINI YA UTEKELEZAJI MALENGO YA MWAKA

0

Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Dkt.  Leonard Akwilapo,akizungumza wakati akifungua mkutano wa mwaka wa tathmini uliowakutanisha wizara ya Elimu na wadau wengine wa elimu pamoja na asasi za kiraia jijini Dodoma. 

mwenyekiti wa mtandao wa Asasi za kiraia ambao ni wadau wa elimu, TENMET, ambaye pia ni Mkurugenzi wa Hakielimu,Dr. John Kalage,akitoa taarifa katika mkutano wa mwaka wa tathmini uliowakutanisha wizara ya Elimu na wadau wengine wa elimu pamoja na asasi za kiraia jijini Dodoma. 

Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa  anayeshughulikia afya Dkt. Dorothy Gwajima,akizungumza kwenye mkutano wa mwaka wa tathmini uliowakutanisha wizara ya Elimu na wadau jijini Dodoma kwa ajili ya kujadili kwa pamoja.

Muwakilishi wa wadau wa maendeleo kutoka DFID UK,Natalie Smith,akizungumza wakati wa ufunguzi wa mkutano wa mwaka wa tathmini uliowakutanisha wizara ya Elimu na wadau wengine wa elimu pamoja na asasi za kiraia ambazo ni wadau wa elimu.

Sehemu ya wadau wakifatilia ufunguzi wa mkutano wa mwaka wa tathmini uliowakutanisha wizara ya Elimu na wadau wengine wa elimu pamoja na asasi za kiraia ambazo ni wadau wa elimu, na wafadhili unaofanyika jijini Dodoma kwa siku tatu.

Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa  anayeshughulikia afya Dkt. Dorothy Gwajima,akimkabidhi  Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Dkt.  Leonard Akwilapo,Tuzo ya Africa Techoology Challenges ambapo Tanzania imepewa baada ya kushika nafasi ya pili katika Mashindano hayo.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Dkt.  Leonard Akwilapo,akionyesha juu tuzo ya Africa Techoology Challenges ambapo Tanzania imepewa baada ya kushika nafasi ya pili katika Mashindano hayo.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Dkt.  Leonard Akwilapo,akimkabidhi certificate mwanafunzi aliyefanya vizuri katika mashindano ya Africa Techoology Challenges,ambapo Tanzania imeshika nafasi ya pili.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Dkt.  Leonard Akwilapo,akimkabidhi certificate Mkufunzi wa chuo cha DIT baada ya kuisaidia Tanzania kushika nafasi ya pili mashindano ya Africa Techoology Challenges.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Dkt.  Leonard Akwilapo akiwa katika picha ya pamoja na wadau wa Elimu.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Dkt.  Leonard Akwilapo akiwa katika picha ya pamoja na wanafunzi waliofanya vizuri katika mashindano ya Africa Techoology Challenges ambapo Tanzania imeshika nafasi ya pili.

PICHA ZOTE NA ALEX SONNA-FULLSHANGWEBLOG

……………………

Na.Alex Sonna,Dodoma

Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Dkt.  Leonard Akwilapo, amesema serikali imekuwa ikifanya kila jitihada kuhakikisha inaboresha hali ya Elimu hapa nchini ikiwa ni pamoja na kuboresha miundombinu na kupitia mitaala kama inatija kwa wakati wa Sasa.

Dkt Akwilapo ameyasema hayo leo Jijini Dodoma wakati akifungua mkutano wa mwaka wa tathmini uliowakutanisha wizara ya Elimu na wadau wengine wa elimu pamoja na asasi za kiraia ambazo ni wadau wa elimu, na wafadhili wanaokutana kwa siku tatu kutoa taarifa na kutathmini malengo waliojiwekea katika kuboresha elimu.

Amesema Wizara imekuwa ikifanya jitihada za maksudi kuhakikisha kiwango cha elimu kinakuwa na kutoa elimu yenye ubora, na wameanza kuboresha miondombinu ya vyuo ya Elimu ya juu, Kati na shule zote msingi na sekondari ili maboresho hayo yaendane na miondombinu ili kufanikisha adhima hiyo.

“Serikali tumekuwa tukijitahidi kuboresha hali ya Elimu yetu, utaona kwa Sasa tumeanza kuboresha miondombinu ili tunapotaka elimu iwe bora na miondombinu iwe bora kwa wanafunzi wetu, utaona tumeboresha vyuo vya Mzumbe, UDSM, sambamba na uboreshaji Madarasa kwa vyuo vya Kati na shule zetu zote” amesema Dkt Akwilapo.

Pia amebainisha maboresho hayo yanaenda sambamba na mitaala katika shule zetu na vyuo tunataka iendane na matakwa ya wakati wa sasa ili mwanafunzi anapotoka aweze kujitegemea tofauti na sasa wanategemea kuajiriwa.

Amesema kupitia mkutano huo kwa kushirikisha na wadau hao watajadili na kutoa taarifa ya utekelezaji wa malengo waliojiwekea katika mkutano uliopita, kwa kuangalia mafanikio na  changamoto katika kutekeleza malengo hayo.

Kuhusu kiwango cha elimu hapa nchini amesema imeimalika tofauti na mawazo ya watu wanaofikilia kuwa ipo chini, amesema kwa wanafunzi wanaomaliza sekondari hapa nchini akienda nje kwa elimu ya juu wanafanya vizuri,hata katika mashindano mbalimbali ya nje ya nchi wanafunzi wa Tanzania wamekuwa wakifanya vizuri.

Aidha ametumia mda huo kuwapongeza wanafunzi wa wawili wa chuo cha DIT, waliofanya vizuri na kuiwakilisha nchi katika mashindano ya Africa Techoology Challenges, ambapo Kama nchi tulishika nafasi ya pili kati ya nchi  za Afrika, na kwa mtu mmojammoja, Christopher Mbembela, alishika nafasi ya pili, na Apollo Maturo kushika nafasi ya tatu kati ya wanafunzi wa nchi zilizoshiriki mashindano hayo.

Kwa upande wake mwenyekiti wa mtandao wa Asasi za kiraia ambao ni wadau wa elimu, TENMET, ambaye pia ni Mkurugenzi wa Hakielimu, John Kalage, amesema wao kama wadau wa elimu wanaridhishwa na hali ya Elimu hapa nchini hasa katika udahili kwa wanafunzi msingi umeongezeka, hata wale wa msingi kwenda sekondari.

” Sisi Kama wadau wa elimu tunaipongeza Sana serikali kwa kuamua kutoa elimu bite hii imeongeza sana kuongeza hamasa kwa watoto kusoma, hata ukiangalia usawa wa kijinsia katika udahili sasa unaridhisha Sana kwa sasa” amesema Kalaghe.

Amesema wao kama wadau kupitia mkutano huo wataangalia na kushirikishana changamoto zilizopo katika elimu hasa kuangalia kuongezeka kwa udahili katika shule kusiathiri kutolewa kwa elimu iliyobora kwa watoto wetu.