Home Mchanganyiko VIONGOZI WATAKIWA KUTATUA MIGOGORO YA WANANCHI

VIONGOZI WATAKIWA KUTATUA MIGOGORO YA WANANCHI

0

Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Mpanda Abel Kimazi akizungumza na viongozi wa chama hicho wilaya ya Mpanda katika mkutano wa kawaida wa Halmashauri Kuu ya wilaya

Baadhi ya viongozi kutoka CHADEMA wakiwa katika picha ya pamoja na Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Mpanda mara baada ya kujiunga na chama hicho

……………

Na Mwandishi wetu, Katavi

Katika kuelekea uchaguzi wa serikali za mitaa Chama Cha Mapinduzi wilaya ya Mpanda mkoani Katavi kimewataka watendaji wa ngazi mbalimbali katika chama kufanya kazi kwa kushirikiana katika kuondoa migogoro isiyo ya lazima hasa migogoro ya ardhi ambayo imekithiri katika maeneo mengi

Akizungumza na viongozi wa ngazi mbalimbali wa chama hicho, Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Mpanda Abel Kimazi aliwataka kushirikina na viongozi wa serikali katika kutatua migogoro

“Tukiendekeza migogoro hii tutafeli, na lengo la chama chochote cha siasa ni kushinda nasi tunataka kushinda” alisema

 

Aidha aliwataka kutokuvibeza vyama vidogo na kufananisha ushindani kuwa kama vita hivyo haipaswi kumdharau adui

Naye Katibu wa CCM wilaya ya Mpanda Abdallah Kazwika  alisema kwa kipindi cha kuanzia januari mwaka huu hadi sasa wamepokea wanachama wapya 128  kutoka katika vyama vya upinzani

 

Pia katika mkutano huo lilifanyika zoezi la kupokea wanachama wapya watatu waliokuwa viongozi wa nafasi mbalimbali katika chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA

 

Kwa upande wao baadhi ya viongozi waliohama vyama vyao vya siasa na kujiunga na CCM walisema wameridhishwa na utendaji wa serikali ya awamu ya tano