Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Mpanda Abel Kimazi akizungumza na viongozi wa chama hicho wilaya ya Mpanda katika mkutano wa kawaida wa Halmashauri Kuu ya wilaya
Baadhi ya viongozi kutoka CHADEMA wakiwa katika picha ya pamoja na Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Mpanda mara baada ya kujiunga na chama hicho
……………
Na Mwandishi wetu, Katavi
Katika kuelekea uchaguzi wa serikali za mitaa Chama Cha Mapinduzi wilaya ya Mpanda mkoani Katavi kimewataka watendaji wa ngazi mbalimbali katika chama kufanya kazi kwa kushirikiana katika kuondoa migogoro isiyo ya lazima hasa migogoro ya ardhi ambayo imekithiri katika maeneo mengi
Akizungumza na viongozi wa ngazi mbalimbali wa chama hicho, Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Mpanda Abel Kimazi aliwataka kushirikina na viongozi wa serikali katika kutatua migogoro
“Tukiendekeza migogoro hii tutafeli, na lengo la chama chochote cha siasa ni kushinda nasi tunataka kushinda” alisema
Aidha aliwataka kutokuvibeza vyama vidogo na kufananisha ushindani kuwa kama vita hivyo haipaswi kumdharau adui
Naye Katibu wa CCM wilaya ya Mpanda Abdallah Kazwika alisema kwa kipindi cha kuanzia januari mwaka huu hadi sasa wamepokea wanachama wapya 128 kutoka katika vyama vya upinzani
Pia katika mkutano huo lilifanyika zoezi la kupokea wanachama wapya watatu waliokuwa viongozi wa nafasi mbalimbali katika chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA
Kwa upande wao baadhi ya viongozi waliohama vyama vyao vya siasa na kujiunga na CCM walisema wameridhishwa na utendaji wa serikali ya awamu ya tano