********************************
Dar es Salaam- 23 Septemba, 2019
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, chini ya Uongozi
madhubuti wa Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania; imedhamiria kuhakikisha kuwa biashara za
mipakani zinaimarishwa na kufanyika kwa ufanisi zaidi kwa kuondoa
vikwazo vyote vya kikodi na visivyokuwa vya kikodi na kuwezesha
Wananchi na Taifa kwa ujumla kunufaika na kukuza biashara.
Katika kufikia malengo hayo, Wizara ya Viwanda na Biashara inapenda
kuutaarifu Umma na Wafanyabiashara wote nchini hususan wale
wanaofanya biashara mipakani kuwa, imeweka utaratibu maalum
utakaowezesha kutoa taarifa juu ya vikwazo, changamoto au kero za
kibiashara hasa zile zisizokuwa za kikodi (NTBs) wanazokumbana nazo.
Lengo la kuweka utaratibu huu ni kuwezesha wafanyabiashara kupata
huduma haraka kupitia Wizara na Taasisi mbalimbali za Serikali zinazotoa
huduma mipakani. Kwa kuanzia, Wizara imetoa anuani maalumu za barua
pepe na namba za simu za watendaji ambazo tutapenda kila
mfanyabiashara anayepata vikwazo aweze kutoa taarifa kupitia namba
hizo. Aidha, Wizara inawataka Wakuu wa Taasisi hizo walioko kwenye
vituo vya mipakani kubandika orodha hiyo kwenye mbao za matangazo ili
kurahisha mawasiliano. Vikwazo visivyokuwa vya kikodi ni pamoja na:
rushwa ya kifedha na isiyo ya kifedha, urasimu na kutotoa miongozo ya
taratibu zinazohitajika, kukosa taarifa muhimu na kutojua fursa zilizopo.
Kwa upande wa Wizara, taarifa hizo zinapaswa kutumwa kwa Mratibu wa
Vikwazo Visivyo vya Kiushuru (NTB’s) Bi Aneth Simwela kupitia barua
pepe ifuatayo; [email protected] au piga simu namba
+255622259341.
Kwa changamoto za masuala ya Viwanda na Masoko, Wafanyabiashara
na Wadau wanaweza kuwasilisha changamoto zao kupitia barua pepe
[email protected] au kuwasiliana na Bw. Andrew Shirima wa
Wizara ya Viwanda na Biashara kupitia namba ya simu +255713500532.
Wizara na Taasisi ambazo zinazotoa huduma mipakani ni pamoja na:
Mamlaka ya Mapato (TRA); Idara ya Uhamiaji; Wakala wa Vipimo (TBS);
Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA); Mkemia Mkuu wa Serikali; Tume
ya Nguvu za Atomiki Tanzania (TAEC); Kitengo ya Huduma za Afya ya
Mimea; Idara za Maliasili na Utalii, Idara za Mifugo na Uvuvi Halmashauri
za Wilaya na Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade).
Orodha yenye majina ya Taasisi/Mamlaka na mawasiliano ya Maafisa
Wasimamizi wa Taasisi hizo kwa huduma za mipakani inapatikana kwenye
tovuti ya Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade)
www.tantrade.go.tz au kupitia barua pepe: [email protected] au
[email protected] au wasiliana na Bw. John Fwalo kupitia namba
ya simu +255767285252.
Endapo hutaridhika na huduma kutoka Taasisi yeyote tajwa hapo juu,
wasilisha malalamiko yako kwa barua pepe [email protected] au
[email protected] . Unaombwa pia kutumia barua pepe tajwa endapo
utaridhika na huduma zilizotolewa.