Mwakilishi wa Katibu Mkuu wa Wizara ya Malisili na Utalii ,William Mwita akizungumza wakati wa hafla fupi ya kuwaaga wawakilishi wanne wa matamasha ya JAMAFEST na URITHI FESTIVAL wakati wakianza safario ya kupanda Mlima Kilimanjaro kama sehemu ya matamasha hayo yaliyozinduliwa leo na Makamu wa Rais,Mama Samia Suluhu Hassan .
Wawakilishi matamasha makubwa kwa nchi za Afrika Mashariki kutoka kushoto Joel Acana kutoka nchini
Uganda,Anita Brown wa Tanzania
,Luca Waiganja kutoka nchini Kenya
wanao wakilisha tamasha la JAMAFEST na kulia ni Jocktan Makeke akiwakilisha tamasha la
Urithi Festival wakijiandaa na safari ya kupanda Mlima Kilimanjaro.

Mwakilishi wa Kamishna Mkuu wa Uhifadhi wa shirika la
Hifadhi za Taifa (TANAPA) ,Victor Kitansi akizungumza wakati wa kuwaaga wawakilishi hao.

Kaimu Mkuu wa Hifadhi ya Taifa ya Mlima Kilimanjaro,Saimoni Aweda akizungumza kabla ya safari ya kupanda Mlima Kilimanjaro kwa wawakilishi hao wa matamasha ya JAMAFEST na URITHI FESTIVAL kuanza safari ya kupanda Mlima Kilimanjaro.
Mkurugenzi wa Kampuni ya Africanspoonbill tours Pius Momburi (kushoto) akiwa na waongoza wageni katika safari ya wawakilishi wa matamasha hayo,kampuni hiyo ndio imepewa jukumu la kupandisha ugeni huo mlima Kilimanjaro.
Mwakislihi wa tamasha la Urithi Festival ,Jocktan Makeke akieleza matarajio yake katika safari ya kupanda Mlima Kilimanjaro.
Wawakilishi wa matamasha ya JAMAFETS na URITHI FESTIVAL wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa Hifadhi ya Taifa ya Milima Kilimanjaro na wawakilishi wa wizara ya Maliasili na Utalii kabla ya kuanza safari ya kupanda Mlima Kilimanjaro.
Na Dixon Busagaga ,Moshi
WAWAKILISHI wanne kutoka nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki
katika matamasha JAMAFEST na URITHI FESTIVAL wameanza safari ya siku sita ya
kupanda Mlima Kilimanjaro kuelekea kilele cha Uhuru ikiwa ni sehemu ya
matamasha hayo yaliyozinduliwa jana na Makamu wa Rais,Mh Samia Suluhu Hassan.

Wanaopanda Mlima Kilimanjaro kama sehemu ya matamasha hayo
makubwa kwa nchi za Afrika Mashariki ni pamoja na Joel Acana kutoka nchini
Uganda,Luca Waiganja kutoka nchini Kenya na Anita Brown wa Tanzania
wakiwakilisha tamasha la JAMAFEST huku Jocktan Makeke akiwakilisha tamasha la
Urithi Festival.

Safari
ya wawakilishi hao mbali na kuwa sehemu ya kuanza rasmi kwa matamasha
haya mawili pia ,wanapanda kwa leongo kupeleka ujumbe kupitia Ngao za
Urithi Festival unaosema “Celebrating Our Heritage” na ule wa JAMAFEST .

Akizungumza wakati wa hafla ya kuwaaga washiriki
hao,Mwakilishi wa Katibu Mkuu ,Wizara ya Maliasili na Utalii,William Mwita
alisema chanzo cha tamasha la JAMAFEST ni utekelezaji wa maelekezo ya
sekretarieti ya Jumuiya ya Afrika Mashariki ya kutaka Malikale na Utamaduni
kutumika kama vivutio vya Utalii.

“Sekretarieti ilizielekeza nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki mwaka 2012
zihakikishe Malikale na utamaduni unatumika kama kivutio cha utalii ili uweze
kutumika katika maendeleo ay nchi za afrika Mashariki .”alisema Mwita.

Alisema baada ya maelekeozo hayo ,sekretarieti ilianzisha tamasha la Sanaa na Utamaduni kwa nchi za
Afrika Mashariki likiwa tayari
limefanyika katika nchi tatu,Kigali (Rwanda) ,Nairobi (Kenya) ,Kampala (Uganda)
na sasa linafanyika Dar es Salaam Tanzania .

Kwa Tanzania ,tamasha la JAMAFEST limezinduliwa jana katika
uwanja wa Taifa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ,Mh Samia
Suluhu Hassan sambamba na tamasha la URITHI FESTIVAL ,tamasha ambalo liko
kwenye ngazi ya kitaifa likiwa na maudhui kama ya tamasha la JAMA FEST.

“Sambamba na tamasha la JAMAFEST pia linafanyika tamasha la URITHI
FESTIVAL , ni kwamba Tanzania imekuwa ya kwanza kutekeleza maelekezo ya Jumuiya
ya Afrika Mashariki ya kuhakikisha Mali kale na Utamaduni vinatumika kama
vivutio vya utalii hivyo Tanzania ikaanzisha tamasha hili la URITHI FESTIVAL likiwa katika ngazi ya kitaifa.”

Wakati Jamafest inaunganisha wana Afrika Mashariki na
kutumika kama kivutio cha Utalii au zao la utalii ,Urithi FESTIVAL INAFANYA
mambo hay ohayo kwa Tanzania,kamba unaunganisha Watanzania na inatumika kama
zao la Utalii.

“Tamasha limeanza leo (Jana) kutakuwa na ngoma za asili ,michezo ,maigizo
,kutakuwa na Nyama Choma Pori wale wanaopenda kula nyama ya Mamba,Kiboko na wanyama
pori wengine ni wakati wao katika matamasha haya .”alisema Mwita .

Alisema Tamasha la JAMAFEST litafanyika kwa siku nane huku
tamasha la Urithi Festival likiendelea kufanyika katika mikoa 12 ya Tanzania Bara
ambayo imepewa kutangaza kivutio ambacho kitatumika kama zao la Utalii katika
maeneo yao.

Mapema mwakilishi wa Kamishna Mkuu wa Uhifadhi wa shirika la
Hifadhi za Taifa (TANAPA) ,Victor Kitansi aliwakapongeza waratibu wa matamasha
hayo kufanya uamuzi wa kutumia sehemu ya matukio kuwa ni kushiriki kupanda
Mlima Kilimanjaro.

Tamasha la JAMAFEST ambalo hufanyika kila baada ya miaka
miwili kuzunguka nchi wanachama linafanyika kwa muda wa siku nane huku Tamasha
la Urithi Festiva likifanyika katika mikoa 12 ya Tanzania Bara kwa kila mkoa
kuionesha kivutio ambacho kitatumika kama zao la Utalii.

Mwisho .