KAIMU Mkurugenzi wa Menejimenti ya Maarifa Costech Emanuel Abiner akisalimiana na mmoja wa watafiti kwenye wa Taasisi ya Mifugo Tanzania (Taliri) wakati alipowasili eneo hilo
Afisa Utafiti Mkuu Kiongozi Dkt. Bakari Msangi akiwa kwenye eneo hilo
TAASISI ya ya utafiti wa mifugo Tanzania (TALIRI) inayojihusisha na utafiti wa malisho bora ya mifugo imesema imekuja na teknolojia mbalimbali za malisho ili kupunguza migogoro baina ya wakulima na wafugaji katika kipindi cha kiangazi ili kukomesha migogoro hiyo.
Kauli hiyo imetolewa na Kaimu Mkurugenzi kutoka taasisi ya utafiti wa mifugo Tanzania Dkt. Zablon Nziku wakati tume ya Taifa ya sayansi na teknolojia (COSTECH) ilipofanya ziara na waandishi wa habari kutoka Mikoa ya Tanga, Morogoro na pwani ya kutembelea na kujionea namna taasisi za utafiti zinavyofanya kazi zake.
Dkt Nziku alisema kumekuwepo na migogoro mingi hususani kipindi cha malisho kuhusiana na ukosefu wa malisho katika kipindi cha kiangazi hivyo wamekuja na teknolojia ya kuhifadhi malisho ili mfugaji aweze kuwa na uhakika wa upatikanaji wa chakula cha mifugo kwa mwaka mzima.
Alisema moja ya teknolojia waliyokuja nayo ni pamoja na kufunga aina ya malisho yakiwa makavu kwa kuhifadhi ambapo mnyama anaweza kuyatumia kama chakula kipindi cha kiangazi na hata masika kitendo
kitakachowawezesha wafugaji kupata maziwa mengi wakati wote.
Alisema kuwa mbadala wa malisho hayo utasaidia kupunguza kuvamiwa kwa mashamba ya serikali kwani kwani zipo teknolijia zinazoweza kutumika hata kwa mtu mmoja mmoja ili kuongeza ufanisi.
Dkt Nziku alisema endapo wafugaji wengi watafanikiwa kupanda aina hiyo ya malisho bora tija kwenye maziwa itaongezeka na hatimaye viwanda vitapata malighafi za kutosha hivyo ipo haja ya wafugaji kuchangamkia fursa hiyo.
‘’Kiwanda chetu cha kuchakata maziwa cha Tanga fresh kinatumia maji kusafisha mitambo yao ambapo kwa siku wanalita laki moja na 20 ambapo maji wanayosafisha tumeona kuliko wayatupe wanayatrit ya kuyarudishiauhai ambapo sisi tunayatumia kumwagilia hili eneo la mfano kwajili kupata mbegu hizi,’’alibainisha Dkt Nziku.
Kwa upande wake Afisa utafiti mkuu kiongozi Dkt. Bakari Msangi alisema wao kama tume ya Taifa ya sayansi na teknolojia kuanzia mwaka 2012 mpaka sasa wametoa bilioni 47 kwa taasisi mbalimbali za kitafiti kwajili ya kufanyia shughuli za kiutafiti ambapo kila mwaka wanatoa takribani bilioni 18-20 kwa miradi mbalimbali kutoka kwenye taasisi tofauti tofauti kulingana na namna walivyoshindanishwa.
Alisema matokeo chanya yanayofanywa na taasisi hiyo yanazidi kuwafanya wafadhili kuwa na motisha ya kuendelea kutoa ufadhili wao ambapo watafiti wamekuwa wakizitumia katika miradi ya kiutafiti.
Alisema jukumu la tume ni kuhakikisha wanasaidia tafiti na ubunifu kufanyika katika taasisi mbalimbali zikiwemo za utafiti na vyuo vya elimu ya juu na kati ya mambo wanayoyafanya ni pamoja na kuwajengea uwezo watafiti lakini pia kujenga vyema miundombinu ya kiutafitiikiwemo maabara lakini pia sehemu za mashamba.
Kwa upande wake Salvatory Kavishe kutoka kitengo cha malisho TALIRI alisema ni kuhakikisha wanapata mbegu za kutosha ili waweze kuwauzia wakulima ambao ni wafugaji ilin kuachana na ufugaji wa mazoea.
Alisema wametembea katika mikoa 10 Nchini kwajili ya kuchukua majani na kuyakusanya ambayo watayaboresha na kuwa mbegu bora ambapo kila mkoa wamechukua mbegu tatu tatu ili kuzifanyia utafiti ulionekana kuwa na matokeo makubwa.