Mtendaji wa Mahakama Kuu Kanda ya Tanga, Bw. Ahmed Ng’eni,(aliyeinama) ambaye amemwakilisha Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania,akigagua sehemu ya kukaa maabusu ya Mahakama ya Mwanzo Magoma, iliyopo Korogwe mkoani Tanga, wakati wa makabidhiano ya ujenzi wa Mahakama hiyo yaliyofanyika Septemba 19, mwaka huu. Makabidhiano hayo yalihusisha Mkandarasi – SUMA JKT Kanda ya Kaskazini, Mshitiri – Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania aliyewakilishwa na Mtendaji wa Mahakama Kuu Kanda ya Tanga, Mshauri elekezi wa Mradi – Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) Mkoa wa Tanga pamoja na Mshauri mdogo wa umeme na Mitambo (TEMESA) Mkoa wa Tanga.
Mkadiliaji Majenzi (QS) Yassin Khatib (mwenye shati nyeupe) kutoka TBA, akielezea jambo wakati wa makabidhiano hayo.
Mtendaji wa Mahakama Kuu Kanda ya Tanga,Bw. Ahmed N’geni (kulia wa tatu) na Kapteni E. P. Mapunda, ambaye ni Mwakilishi wa Meneja wa Kanda SUMA JKT wakitia saini makabidhiano hayo na wa pili kushoto ni Mkadiliaji Majenzi (QS) Yassin Khatib (mwenye shati nyeupe) kutoka TBA. (Kulia wa pili) ni Afisa Utumishi wa Mahakama Kuu Tanga, Bw. Faridi Mnyamike, akifuatiwa na Mlinzi wa Mahakama ya Mwanzo Magoma, Bw. Miraji Sufian.
Mtendaji Mkuu wa Mahakama Kuu Tanga, Bw. Ahmed N’geni(katikati) akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wengine, ambao wapili kulia ni Kaimu Naibu Msajili wa Mahakama Kuu Tanga, Mhe. Cassian Matembele na wa kwanza kulia ni Afisa Utumishi wa Mahakama Kuu Tanga, Bw. Faridi Mnyamike. Kushoto ni Afisa Tawala wa Mahakama ya Wilaya Korogwe, Bw. Emmauel Machimo akifuatiwa na Kapteni E. P. Mapunda.
Muonekano wa jengo la Mahakama ya Mwanzo Magoma.
Muonekano wa ndani wa jengo la Mahakama ya Mwanzo Magoma.
(Picha na Amina Ahmad – Tanga)