******************************
Na. Kwiyeya Singu
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Ndg. Paul Makonda halali bila kuhisi sauti ya Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ndg. Dk. John Pombe Magufuli ikimsemesha.
Ni katika tafakuri juu ya miradi ya kimkakati inayopigishwa maktaim na wasaidizi wake ambayo kimsingi ni miingoni mwa ahadi ya Rais Magufuli wakati wa Kampeni zake.
Mkuu wa Mkoa Paul Makonda kwa kulitambua hilo, inasemekana kwamba, anatarajia kuhitisha Mkutano mkubwa wa dharura wa kimkoa utakaohusisha Wakuu wa Wilaya wote wa Mkoa huo, Wakurugenzi na Wakandarasi wanaoendelea na ujenzi wa miradi mbalimbali katika Mkoa huo ili kufanya tathmini ya yaliyotokea katika Ziara ya Rais Magufuli iliyopita. Ni maamuzi ya busara sana kwa kiongozi anayeumizwa na shida za watu wake, ni jambo la kutambua wananchi umuhimu wa kumuunga mkono Mkuu wao kwa ajili ya maendeleo yao pia.
Ikumbukwe kuwa, mwaka 2016 Mkuu huyo Paul Makonda katika ziara yake maarufu kama ‘tumbua tumbua ya Makonda’ au ujenzi wa “Dar Mpya” aliagiza kukamatwa kwa watendaji 6 na kuwaweka ndani baada ya kuwa wanakwamisha kutatua migogoro ya ardhi kule Magwepande. Sambamba na hilo, Makonda aliwahi kuwasimamisha wajenzi na Wakandarasi waliokuwa wanaharibu barabara za jijini hilo uliokuwa ukisababisha mashimo mengi hadi hapo wakandarasi hao walipofuata taratibu zote za ujenzi na kufanya barabara kuwa nzuri.
Katika nchi hii, kwa tulipofikia, ziara za Makonda zilizoacha shangwe kubwa kwa wakazi wa Dar hadi Makonda kuonekana lulu na kuwa mfano kwa wakuu wengine, lakini wapo watu pia walisema ya kusema, kwa hisia zao, na mitazamo yao waliyohisi wako sahihi, wakoaji hao walimkosoa Makonda kwamba kutumbuatumbua huko kunamjengea taswira mbaya kama kiongozi, wakasema huo ni ulevi wa Madaraka. Wakosoaji wake hawakujua ya wahenga waliposema “ukicheka na Nyani utavuna Mabua”.
Kwa kuwa uongozi ni wa watu, kuna wakati mwingine humtaka kiongozi asikilize watu baada ya fikra au mawazo yake kukutana na hoja pinzani wakati wa utekelezwaji wake.
Ikabidi Makonda akae kimya, pengine kwa kuyaheshimu mawazo ya wengine ikambidi kusikiliza maoni na mitazamo mingine ya watu wanaompinga.
Makonda aliamua kukaa kimya kwa kuwaacha kwa muda watumishi akijua kuwa, kwanza kwa sababu ya wakosoaji wake waliodhani uongozi ni jambo la mchezo mchezo bila vision.
Pili, ni kwa sababu ya utawala wa sheria na kwamba huenda watasimama vizuri na kujiendesha kama ambavyo taratibu, kanuni zinavyowaruhusu, lakini wapi, matokeo yake ni ni dalili ya kuambulia mabua mfano huko coco na machinjio ambapo si tu kukwamisha maendeleo ya wananchi, bali pia ni kumsononesha Rais wa Nchi Dk. Magufuli ambaye ndiye mwenye dhamana kubwa ya Maendeleo ya Watanzania.
Kwenye hili naamini kabisa kwamba RC. Makonda hatanii na bahati mbaya hajawahi kuleta utani ktk masuala ya msingi, anaheshimu shughuli za wananchi.
Makonda anatambua kuwa coco ilimilikiwa kibinafsi na wenye hila maarufu kama Vigogo, na ikumbukwe kuwa Makonda alianza kuipambania coco wakati akiwa Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni hadi Rais Magufuli alipoingia madarakani na kuendeleza mapambano hayo hadi kufanikisha kuirejesha.
Baada ya hapo Rais JPM akatenga fedha kwa ajili ya Ujenzi wa Coco, na Mradi wa Machinjio nk.
Soko la Kisutu, Machinjio ni miongoni mwa miradi muhimu anayoitajataja Mkuu wa Mkoa huyo. Makonda anasema, Dar es Salaam na Tanzania kwa ujumla ni nchi ya pili Afrika na duniani kote kwa kuwa na Ng’ombe wengi kuliko nchi nyingine lakini nyama zinazouzwa Supermarket na nyama zinazouzwa mahoteli makubwa zote zinatoka nje ya nchi wakati sisi Tanzania ni matajiri wa Ng’ombe kuliko huko zinakotokea nyama hizo.
Makonda anasema, Nyama, Ngozi zetu za Ng’ombe, Kwato, Pembe kutokuwa na soko nje ya nchi ni kwa sababu ya mfumo tunaotumia katika uchunaji.
Hivyo, tarehe 25/9/2019 inayotajwa kufanyika kwa mkutano wa dharura, itakuwa ni tarehe ya kila kiongozi katika Mkoa wa Dar es Salaam kubeba mzigo wake badala ya kumtwisha mizigo hiyo ya dhambi Mkuu wa Mkoa wa Dar Paul Makonda.
Nampongeza sana RC. Paul Makonda kwa hatua hii ya kuhitisha kikao cha dharura ili kuyapatia majibu yanayochafua taswira na jitihada za Mkuu wa Mkoa hususan Rais wa nchi Dk. Magufuli kuhusu maendeleo ya wananchi kwa sababu ya watumishi wachache. Siku zote nasema, ukitaka kuepuka nzi tupa kibudu, Mkuu Makonda simamia ukweli hata kama utabaki peke yako unayeamini katika ukweli. RC tupa kibudu.
Potelea popote, liwalo na liwe ilimradi hatua zozote zitakazochukuliwa zinalenga maslahi ya watanzania wa Dar es Salaam, Maendeleo ambayo yanayonekana kwa macho na vitendo vya viongozi na sio maneno maneno tu. Hayo ndiyo wanayataka wananchi wetu. Potelea popote liwalo na liwe.
Kama haiwezekani kuogopwa na kupendwa kwa wakati mmoja, basi ni heri uogopwe kuliko ukapendwa. Makonda ni muhimu sana kuepukana na kuvuna mabua kwa kuwachekea hao wanaokwamisha miradi ya kimkakati katika nchi yetu. Jambo jingine ni kwamba, Jiji la Dar es Salaam ndipo ilipo sura ya nchi, Dar inaitwa Tanzania kutokana na mji huo ulivyo wageni wengi kutoka nje ya nchi wanawatambua Watanzania kupitia picha wanayoiona jijini humo. Narudia tena kusema kwamba, kama haiwezekani kuogopwa na kupendwa kwa wakati mmoja, ni heri uongopwe kuliko ukapendwa. Ni jambo jema sana kwa Kiongozi wa Mkoa kama wa Dar es Salaam kuogopwa kuliko kupendwa.
Jenerali Ngwilizi aliyewahi kuwa Mkuu wa Mkoa huo wa Dar aliipeleka Dar Kijeshi.
Sanaa ya Uongozi au sifa ya Kiongozi mzuri ni uwezo wa kusema ‘hapana’ na si ‘ndiyo’.
Katika hili binafsi sina shaka na misimamo ya Paul Makonda ambaye ndiye Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, hili Jiji bila ya Makonda lingekuwa la hovyo sana mpaka sasa.
Tungetamani sana uendelee kuinyoosha Dar lakini wananchi wengi wanakuhitaji kwenye majimbo yao, huenda wanayo ya moyoni kuhusu Taifa letu. Watakwambia muda ukifika.