Home Mchanganyiko Viwanja vya ndege kukuza utalii Nyanda za Juu Kusini

Viwanja vya ndege kukuza utalii Nyanda za Juu Kusini

0

Katibu Kata ya Nduli mkoani Iringa, Wilbert Chale (kulia) akipata
maelezo ya uboreshaji wa viwanja mbalimbali vya Ndege vilivyopo chini ya
Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania kutoka kwa Ofisa Uhusiano wa
Mamlaka hiyo, Bahati Mollel, alipotembelea banda la maonesho ya Karibu Utalii
Kusini yaliyofunguliwa leo na Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, Dkt. Tulia Akson yanayofanyika kwenye viwanja vya Kihesa-Kilolo

Afisa Usalama wa Kiwanja cha Ndege cha Iringa, Miyaga Juma
(kushoto) akisikiliza maswali ya Meneja wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga wa
Mkoa wa Iringa, Rosalia Makwaya, alipotembelea banda la maonesho la
Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA) ya Karibu Utalii Kusini
yanayofanyika kwenye Viwanja vya Kihesa-Kilolo.

Watumishi wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA)
wakiwa mbele ya banda la maonesho ya Karibu Utalii Kusini, ambayo
yamezinduliwa leo na Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, Dkt. Tulia Akson.

Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Mhe. Albert Chalamila (wa pili kulia) na
Katibu Tawala Mkoa wa Songwe, David Kafulila (kulia), wakimsikiliza Kaimu
Meneja wa Kiwanja cha Ndege cha Iringa, Lydia Mwenisongole (watatu kulia),
akitoa maelezo kuhusiana na viwanja vya ndege wakati walipotembelea banda la
maonesho la Mamlaka hiyo la Karibu Utalii Kusini, yaliyozinduliwa leo na Naibu
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Tulia Akson.

Kaimu Meneja wa Kiwanja cha Ndege cha Iringa, Lydia
Mwenisongole (wa pili kulia) na Meneja wa Mamlaka ya Hali ya Hewa (TMA)
mkoa wa Iringa, Haji Usantu (kulia) wakimsikiliza mgeni rasmi wa maonesho ya
Karibu Utalii Kusini yaliyozinduliwa leo na Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, Dkt. Tulia Akson.

Mhandisi Astelius John (kushoto) akimfafanulia jambo Afisa
Biashara wa Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) mkoa wa Iringa, Winfrida
Kihange, alipotembelea banda la Maonesho la Mamlaka ya Viwanja vya Ndege
Tanzania (TAA) ya Karibu Utalii Kusini yaliyozinduliwa leo na Naibu Spika wa
Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Tulia Akson.

*************************

Na Mwandishi Wetu
UBORESHAJI wa miundombinu ya viwanja vya ndege na barabara kwa Nyanda za Juu Kusini kutachangia kukuza utalii kutokana na kuwa na vivutio vingi zaidi.
Kauli hiyo imetolewa leo na Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, Dkt. Tulia Akson alipozindua maonesho ya Karibu Utalii Kusini yanayofanyika kwenye Viwanja vya Kihesa-Kilolo, ambapo yanashirikisha taasisi za umma na watu binafsi.

Hatahivyo, Dkt. Akson amesema tayari amepata taarifa kuwa kuna matengenezo
makubwa ya kiwanja cha ndege cha Iringa, ili kiweze kuhudumia ndege kubwa zaidi ya Bombardier ambayo inabeba abiria 72.

“Nimesikia hapa mkuu wa mkoa amesema kiwanja chetu cha hapa Iringa kitafanyiwa upanuzi mkubwa wa barabara ya kutua na kuruka ndege, na pia viwanja vya mikoa ya Mbeya, Mpanda, Songea na Katavi vyote vitaboreshwa zaidi,” amesema Dkt. Akson.

Lakini, amewataka wakazi wa Nyanda za Juu Kusini kuwa wabunifu kwa kuvutia watalii kutembelea vivutio vilivyopo, ikiwemo milima mingi, Hifadhi za Taifa za Ruaha, Mikumi, Udzungwa, Katavi na Kitulo; Kimondo cha Mbozi, Maporomoko ya Maji ya Kalambo na Ziwa Ngosi.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Ally Hapi amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. John Pombe Magufuli kwa kufanikisha upanuzi wa jengo la abiria na ukarabati wa barabara ya kutua na kuruka kwa ndege ya kiwanja hicho.

Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS), Mhandisi Patrick
Mfugale amesema barabara ya kwenda kwenye Hifadhi ya Ruaha itaboreshwa, pamoja na Kiwanja cha ndege cha Iringa nacho kipo kwenye mchakato wa maboresho hayo.