Mwenyeketi wa bodi ya Wakurugenzi Vodacom Bw.Ally Mufurukiakiongea na Wanahabari baada ya Mkutano Mkuu wa Wanahisa wa mwaka 2019 kumalizika katika maeneo ya Mlimani City Jijini Dar es Salaam leo.
Sehemu ambayo kumefanyika Mkutano Mkuu wa Wanahisa Vodacom wa mwaka 2019 uliofanyika leo katika maeneo ya Mlimani City Jijini Dar es Salaam.
****************************
NA EMMANUEL MBATILO
Kampuni ya Vodacom Tanzania imepeleka mapendekezo kwa serikali kuona ni namna gani wanaweza kurahisha zoezi la usajili wa laini za simu kwa kutumia mfumo wa usajili wa dole gumba.
Ameyasema hayo leo Mwenyeketi wa bodi ya Wakurugenzi Vodacom Bw.Ally Mufuruki katika Mkutano Mkuu wa Wanahisa uliofanyika Jijini Dar es Salaam.
Akizungumza na Wanahabari, Bw.Mufuriki amesema kuwa kufikia disemba mwaka huu wateja wao wawe wamesajiliwa laini zao kwa mfumo wa dole gumba hivyo lazima uwe na kitambulisho cha uraia ambacho ni changamoto kwa wengi mpaka sasa.
“Tunawateja Milioni 14, jumla milioni 40 wateja wanaotumia simu na taarifa tulizonazo hakuna zaidi vitambulisho milioni 15 ambazo zimetolewa mpaka saizi, kwahiyo kuna watumiaji kama milioni 25 ambao hata wakitaka kujisajili hawana vitambulisho vya NIDA”.Amesema Bw.Mufuriki.
Aidha, Bw.Mufuniki amesema kuwa kati ya wateja wao Milioni 14 mpaka sasa wameweza kusajili wateja Milioni 2 tu kutokana na changamoto iliyopo katika hupatikanaji wa Vitambulisho vya NIDA pamoja na usajili.