Na Silvia Mchuruza,Kagera;
Kufuatia mfumo mpya wa kielekitroniki wa kusajili leseni kwa njia ya mtandao “BRELA” wafanyabiashara wilayani karagwe mkoani kagera wamepewa mafunzo jinsi gani ya kuutumia hili kuondokana na changamoto zilizokuwepo hapo awali.
Hata hivyo afisa biashara kutoka BRELA Bw.Peter Liwa amesema kuwa mfumo huo utawasaidia wafanya biashara kufanya usajili wa makampuni yao kwa haraka zaidi kuliko ilivyokuwa hapo awali.
“Sasa najua kwamba wafanya biashara hawatapa taabu ya kwenda kwenye maofisi kwa ajili ya kutaka leseni pia itawaidia kupunguza mda tofauti na ilivyokuwa nyuma lakini pia watapata kuona taarifa zao kwa haraka zaidi”
Nae mkurugenzi wa utawala na fedha kutoka “BRELA” Bw.Bakari Ally Mketo ameushukuru uongonzi wa wilaya hiyo kwa kupokea vizuri mfumo huo ambao unaenda kutumiwa na wafanyabiasha ikiwa ni agizo kutoka serikalini ambapo BRELA ipo chini ya wizara ya viwanda na biashara inayosimamiwa na Dk.Bashungwa ambae pia ni waziri kutoka karagwe mkoani kagera.
“Kwanza kabisa nipende kumshukuru mkurugenzi wa wilaya hii ya karagwe kutokuwa mgumu wa kuelewa pia mfumo huu unatarajiwa kuanza tarehe 1 /10 mwaka huu”Alisema Bw.Bakari.
Vilevile nae mkurugenzi wa wilaya ya karagwe Edward Kitonka amewasisitiza wafanya biashara kuupokea vizuri mfumo huo wa kielekitroniki ambapo amesema utasaidia zaidi kuchangia mapato ya wilaya na mkoa kwa ujulma ikiwa karagwe ni kati ya wilaya 6 kati ya 185 zinazofanyiwa majaribio nchi nzima.
“Kiukweli hii ni neema imetushikia watu wa karagwe tuna bahati waziri wa viwanda na biashara anatoka karagwe lakini pia wakala wa BRELA wakaiona karagwe inafaa kwenye hizo wilaya 6 za majalibio hakika tutapata nafasi ya kuongeza pato la mkoa lakini pia hii ndio Tanzania tunayoiitaji kwa sasa nishukuru juhudi pia za serikali ya awamu ya tano”
Sambamba na hayo yote wafanyabiashara walioudhuria mafunzo hayo wameipongeza wizara ya viwanda na biashara pamoja na serikali ya awamu ya tano kwa pamoja kutokana na kuona kuwa mfumo wa uliokuwa unatumika hapo awali ulikuwa na changamoto kubwa na kuamua kuanzisha mfumo mwingine.
Pia wamewashukuru wakala wa ” BRELA” kwa kutambua umuhimu wa wafanya biashara wakubwa kwa wadogo kutokana na kuwapatia mafunzo kuhusu mfumo huo mpya na jinsi ya kusajili leseni ya biashara mda wowote na mahari popote nchini hata kwa kutumia simu ya mkononi.