Wajumbe wa mkutano wakiwa katika ukumbi wa mikutano wa Kilimo IV Uliopo wizara ya kilimo mkoani Dodoma mara baada ya wasilisho la mfumo wa AfriFarm wakichangia maoni yao katika kuboresha mfuo huo uliofanyika hivi karibuni
Na BashiriSalum
Dodoma
Shirika la Kimarekani linalojihusisha na miradi mbalimbali ya kilimo na
elimu (project concern international) PCI leo wamewasilisha matokeo
ya matumizi ya mfumo wa Afrifarm katika kupambana na kiwavijeshi
vamizi fall armyworms katika mkutano uliofanyika kwenye ukumbi wa
mikutano wa Kilimo IV Uliopo Dodoma na kuhusisha wataalamu
mbalimbali na baadhi ya viongozi wa Wizara ya Kilimo .
Mfumo huo ambao hutumika Zaidi kwenye simu ganja uliogunduliwa
na Shirila la PCI kwa lengo la kupambana na kiwavijeshi vyamizi katika
Mkoa wa Mara ikihusisha kutoa mafunzo ya utambuzi wa kiwavijeshi
vamizi (FAW identification) ,ukaguzi wa mashamba, FAW field scouting
na kutoa taarifa za kiwango cha mashambulizi katika ngazi ya jamii
husika.
Akiongea wakati wa ufunguzi wa kikao hicho mwakilishi wa Katibu
Mkuu Wizara ya kilimo ambaye ni Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Sera
na Mipango sehemu ya Ukusanyaji wa Taqwimu Bwana… ..Rubboa
amesema shirika hilo kwa kushirikiana na Kitengo cha Huduma ya Afya
ya Mimea (PHS) chini ya Wizara ya Kilimo, Kampuni ya Dimag walifikia
hatua kubwa ya kuvumbua mfumo huo wakielekitroniki unaoitwa
AfriFARM, (Africa fall armyworm Response Mechanism).
Akiuelezea mfumo huo Bwana Luboa amesema kwamba AfriFARM ni
mfumo wa simu (mobile phone application) uliobuniwa ili
kumuwezesha Afisa ugani au mkulima kujifunza juu ya ufahamu wa kiwavijeshi vamizi, ukaguzi wa shamba na mbinu mbalimbali za
kukabiliana na uvamizi huo.
Aidha shirika la PCI limewekeza katika kukuza matumizi ya teknolojia
ambapo lilifanya majaribio katika Kata 45 zilizoko katika wilaya ya
Butiama, Bunda na Musoma vijijni katika Mkoa wa Mara ambako
kulipata athari ya visumbufu vamizi alisema Bwana luboa.
Hata hivyo Bwana Rubuo ametoa wito kwa wataalamu walioshiriki
katika mkutano huo kuahakikisha wanatoa michango yao katika
kuimarisha mfumo huo ambao utasaidia kuimarisha usalama wa
chakula hapa nchini.
Naye Meneja wa Idara ya Kilimo Bwana Amithay Kuhanda Amesema
wameshirikiana na Wizara ya Kilimo katika kupambana na kiwavijeshi
vyamizi ambao wanachangia kushusha kiwango cha uzalishaji wa mazao
ya wakulima.
Anasema kuwa wanapambana na kiwavijeshi kwa kutumia mfumo wa
kielektroniki simu janja ambao una saidia kufanya ufutiliaji wa
mashamba yaliovamiwa na kiwavijeshi na kutoa taarifa kupitia mfumo
wa simu hiyo.
Mfumo huu unafanya kazi zaidi kuanzia ngazi za Kata kufikisha taarifa
ngazi ya wilaya kwa haraka zaidi hiyo kusaidia kutoa taarifa sahihi za
maeneo ambayo yameathirika kwa hatua zaidi.
Mchango washirika hili la PIC ni kuandaa mfumo ambao unasaidia kuwa
tambua viwavijeshi na kufikisha taarifa haraka kwa wataalamu na
watoa maamuzi kwa maaana ya serikali alisema bwana Amithay
Kuhanda.
Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya uendelezaji wa mazao Bwana ….Malema
amelishukuru shirika hilo kwa hatua walizochukua za kupambana na
viwavijeshi vamizi na kuahidi kutoa ushirikiano mkubwa ili kuhakikisha
huduma hiyo inatumika katika mikoa mingi Zaidi.
Bwana malema amesema kwamba mfumo huo utasaidia kupunguza
gharama za ufuatiliaji na ambazo kwa kiasi kikubwa zilichangia
visumbufu hao kuenea kwa kasi katika maeneo mengine
Hata hivyo alimalizia kwa kuwataka wataalamu kujifunza tekinolojia hii
ili kuwasaidia wakulima na kupunguza changamoto ya usafriri katika
maeneoa mbayo yalikuwa hayafikiki kwa urahisi .
Naye kaimu Mkurugenzi wa huduma ya Afya ya mimea Bwana Jubilant
Mwangi amelishukuru Shirika la PCI kwa kujana mfumo wa AfriFarma
mbao utawasaidia sana wakulima .
Ameshauri mfumo huu kutumika maeneo mengi Zaidi hapa nchini kwa
ajili ya kusaidia kupunguza upotevu wa chakula ambao unaweza
kusababisha hasara kwa wakulima wengi.
Aidha amewataka wakulima wote nchini kutumia mbinu husihi kama
IPM mbinu husishi ya visumbufu na kuwa na mitego ambayo
itawakamata kuliko kuongeza matumizi ya madawa yenye kemikali
ambayo yanasababisha kushuka kwa soko la bidhaa husika alisema
bwana Jubilant Mwangi.