Katibu Mkuu Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto (Idara Kuu Afya) Dkt. Zainab Chaula akiongea na Wabunge kutoka Chama cha Wabunge cha Kupambana na Malaria na Magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele Tanzania (TAPAMA) na chama cha wabunge kutoka Uingereza na Ujerumani(hawapo pichani) ambapo wamejadili jinsi ya kupambana na Malaria na NTD nchini Tanzania,kushoto ni Katibu wa TAPAMA Dkt.Raphael Chegeni
Mbunge wa Uingereza Dkt. William akipeana mkono na Katibu Mkuu Dkt. Zainabu Chaula ambapo wabunge kutoka Uingereza na Ujerumani wamewapongeza TAPAMA kwa kushirikia na Wizara ya Afya na TAMISEMI katika mapambano ya magonjwa hayo na kuahidi kuisaidia Tanzania dhidi.ya Malaria na Magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele
Katibu Mkuu Dkt. Chaula akimkabidhi Miongozo na Mikakati ya Wizara ya kupambana na magonjwa hayo nchini Dkt. Chegeni ambapo Serikali ya Tanzania imejiwekea kutokomeza magonjwa hayo ili kuboresha afya ya watanzania nchini.
Mbunge kutoka Uingereza Dkt. Paul William akipokea miongozo ya Wizara ya Afya ya kutokomeza Malaria na NTD nchini.
Baadhi ya Wabunge kutoka Uingereza na Ujerumani wakisikiliza majadiliano katika kikao hicho kilichofanyika kwenye ukumbi wa TAMISEMI mjini Dodoma.
Mwenyekiti wa TAPAMA (kulia) Mhe.Riziki Lulida akiongea kwenye mkutano huo ambapo alisema lengo la kuanzisha chama hicho ni kuona magonjwa hayo yanatokomea nchini kwani bado watoto wadogo wanafariki na Malaria.
**********************************
Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dkt. Zainab Chaula leo amekutana na kufanya majadiliano na Chama cha cha Wabunge wanaopambana na Malaria kutoka Uingereza na Ujerumani pamoja na Wabunge wa Tanzania wa Chama cha kupambana na.Malaria na Magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele(TAPAMA) pamoja na watendaji kutoka wizara ya Afya na TAMISEMI
Katika majadiliano hayo wamekubaliana kushirikiana katika kutokomeza magonjwa hayo hapa nchini ili kuweza kuokoa maisha ya wananchi hususan watoto wadogo
Kwa upande wa Malaria kulingana na mkakati wa mwaka.2015-2020 ulikua na lengo la kupunguza Malaria chini ya asilimia 5 mwaka 2016 na baada ya tathimini wamefanikiwa kupunguza hadi kufikia asilimia 7.3 ikiwa ni lengo la.kufikia asilimia moja mwaka 2020 hivyo wameainisha na kupanga mikakati ya kutokomeza kwa asilimia hiyo.
Na upande wa Magonjwa yaliyokuwa.hayapewi kipaumbele(NTD),Wizara imejikita katika kudhibiti magonjwa matano ikiwemo usubi,minyoo,trakoma,kichocho pamoja na matende na mabusha
Kwa mwaka huu wamefanikiwa kufanya upasuaji wa mabusha kwa watu 1607 na watu 16748 wameweza kurekebishiwa vikope na kuendelea kuona na hivyo kubakiza kuwafikia watu 5923 ambao kwa namna moja hawakuweza kujitokeza kutokana na imani potovu hata hivyo wizara kwa kushirikiana na mpango wa taifa wa kudhibiti magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele wanaendelea kufanya uhamasishaji kupitia vyombo vya habari pamoja na kugawa dawa kwa wananchi