NJOMBE
Imewataka watanzania ifikapo sept 24 kujitokeza kuchagua viongozi katika ngazi za vitongoji na vijiji wenye hofu ya mungu pamoja na kiu ya kutumia vyema na kuzilinda vyema rasilimali za taifa kwa maslahi ya taifa ya wananchi na taifa kwa ujumla.
Akitoa ujumbe wa mwenge wakati wa akiwahutubia wakazi wa kijiji cha Ikuna katika halmashauri ya wilaya ya Njombe Nkwimba Nyangogo ambaye ni miongoni mwa timu ya watu sita wanaokimbiza mwenge huo kitaifa amesema wakati umefika kwa watanzania kuhamasika kwa watu wenye sifa wenye umri wa kuanzia miaka 21 kuchukua fomu na kugombea nafasi mbalimbali za uongozi katika vitongoji na vijiji ili kupata watu wenye sifa watakaomsaidia rais kuifikisha tanzania katika uchumi wa viwanda.
Ngangogo amesema uchaguzi huo ni muhimu na haupaswi kupuuzwa sababu ndiko ambako serikali inaanza kupata walinzi wa amani na rasilimali za taifa kuanzia ngazi ya chini na kwamba endapo watanzania watashiriki ipasavyo taifa litapiga hatua .
Bi Roida Mgulunde ni mkazi wa kijiji cha Ikuna anaupokea ujumbe huo kwa mikono miwili na kueleza kwamba hisia zake kwamba angetamani kuona idadi ya wagombea wanawake ikiongezeka katika chaguzi zote zijazo huku nae akidai yupo tayari kutia nia katika ujumbe .
Awali akipokea mwenge huo kutoka wilayani Wanging’ombe mkuu wa wilaya ya Njombe Ruth Msafiri amesema mwenge huo utazindua miradi 10 yenye thamani ya bil 1.5
Katika mbio hizo mwenge wa uhuru katika hamashauri ya wilaya ya Njombe umefanikiwa kukagua na kuridhishwa na miradi yote kutoka sekta ya elimu na afya na mradi wa maji wa Kidegembie ambao Mzee Mkongea Ally amekataa kuweka jiwe la msingi kwa madai ya kwamba mkandarasi ametumia vifaa vilivyochini ya ubora huku akitoa wiki mbili kwa TAKUKURU kuchunguza mradi huo.