Home Biashara BOT YAKANUSHA KUHUSU TAARIFA YA SARAFU YA SHILINGI 3,000 YA KUMBUKUMBU YA...

BOT YAKANUSHA KUHUSU TAARIFA YA SARAFU YA SHILINGI 3,000 YA KUMBUKUMBU YA VISIWA VYA DOKDO

0

******************************

Benki Kuu ya Tanzania inapenda kukanusha taarifa zinazosambaa mitandaoni
kwamba mwezi Julai 2019 ilitoa sarafu ya kumbukumbu ya visiwa vya Dokdo
yenye thamani ya shilingi 3000. Benki Kuu inapenda kuufahamisha umma kuwa
taarifa hizo si za kweli na kwamba sarafu hiyo siyo mali ya Benki Kuu ya Tanzania
na haijatolewa na Benki Kuu kwa njia yoyote ile na wala Benki Kuu haijawahi
kuingia mkataba na kampuni yoyote kutoa sarafu hiyo.