Home Mchanganyiko MAHAKAMA KUU KANDA YA DAR ES SALAAM YAENDELEA KUTOA ELIMU KWA UMMA

MAHAKAMA KUU KANDA YA DAR ES SALAAM YAENDELEA KUTOA ELIMU KWA UMMA

0

Afisa Utumishi Mwandamizi wa Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, Bw. Fadhili Mbaga (aliyevaa shati la bluu) akitoa elimu kwa umma kuhusu namna ya uendeshaji wa mashauri kwa baadhi ya wananchi waliofika mahakamani hapo leo kwa ajili ya kupata huduma mbalimbali za kimahakama.

Bi. Elizabeth Sendeu Huber (aliyesimmama nyuma) akiuliza kuhusu suala la uhairishwaji wa kesi na kupendekeza utoaji taarifa mapema juu ya  suala hilo, wakati wa utoaji elimu kwa umma, uliofanyika Mahakama Kuu jijini Dar es Salaam leo. 

Hakimu Mkazi wa Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, Mganga Magesa, (aliyevaa suti) akitoa ufafanuzi juu ya upatikanaji wa nakala ya hukumu wakati wa utoaji elimu kwa umma mahakamani hapo leo.

Bw. Yusuph Amiri akiuliza jambo wakati wa utoaji elimu kwa umma ukiendelea mahakamani hapo.

                                                                            (Picha na Aziza Muhali-SJMC)