*****************************
Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linamshikilia mtu mmoja aitwaye WILLIAM
MWAZEMBE [45] Mkazi wa Kijiji cha Ikukwa akiwa na bhangi gramu 300.
Mtuhumiwa alikamatwa tarehe 17 Septemba, 2019 saa 19:30 usiku huko eneo la
Chunya mjini, Kata ya Itewe, Tarafa ya Kiwanja, Wilaya ya Chunya, Mkoa wa
Mbeya katika msako mkali uliofanyika maeneo hayo. Mtuhumiwa ni muuzaji na
mtumiaji wa bhangi. Upelelezi unaendelea.
Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linamshikilia mtu mmoja aitwaye BAHATI NDELE,
[28] Mkazi wa Ilemi akiwa na bhangi kilogram moja [01] na gramu 210.
Mtuhumiwa alikamatwa katika msako uliofanyika tarehe 17 Septemba, 2019 saa
15:30 alasiri huko eneo na Kata Ilemi, Tarafa Sisimba, Jiji la Mbeya. Mtuhumiwa ni
muuzaji na mtumiaji wa bhangi. Upelelezi unaendelea.
Watuhumiwa watafikishwa Mahakamani mara baada ya upelelezi kukamilika.
KUJARIBU KUJIUA KWA KUNYWA SUMU.
Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linamshikilia mwanamke mmoja aitwaye SILVIA
SANDE [28] Mkazi wa Nsongwi kwa mauaji ya mtoto wake mwenyewe aitwaye
ASIFIWE RASHIDI BAINI mwenye umri wa mwaka mmoja na miezi miwili na kwa
jaribio la kujiua yeye mwenyewe kwa kunywa sumu ya kuulia wadudu.
Ni kwamba mnamo tarehe 16 Septemba, 2019 saa 10:00 asubuhi huko Kijiji cha
Nsongwi Juu kilichopo Kata ya Ijombe, Tarafa ya Tembela, Wilaya ya Mbeya Vijijini,
Mkoa wa Mbeya, mtuhumiwa alikunywa sumu ya kuulia wadudu chumbani kwake kwa
lengo la kujiua kisha kumnywesha sumu hiyo mtoto wake aitwaye ASIFIWE RASHIDI
BAINI mwenye umri wa mwaka mmoja na miezi miwili, mkazi wa Nsongwi juu.
Mtuhumiwa na mtoto wake baada ya tukio hilo walikimbizwa kituo cha afya Igawilo
ambapo mtoto alifariki. Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linaendelea kumshikilia
mtuhumiwa kwa mahojiano zaidi na mara baada ya upelelezi kukamilika atafikishwa
Mahakamani. Chanzo cha tukio kinachunguzwa.
KUPATIKANA NA NISHATI YA MAFUTA BILA KIBALI.
Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linawashikilia watuhumiwa tisa [09] kwa tuhuma za
kupatikana na kufanya biashara ya nishati ya mafuta aina ya Diesel na Petrol bila
kibali.
Watuhumiwa wamekamatwa katika msako mkali uliofanywa na Jeshi la Polisi Mkoa
wa Mbeya tarehe 17 Septemba, 2019 katika maeneo ya Maghorofani, Uyole Jijini
Mbeya, Chimala, Igawa na Igurusi Wilayani Mbarali na maeneo mbalimbali ya
Wilaya ya Kyela.
Katika msako huo jumla ya lita 1,500 za Petrol na lita 2,500 za Diesel
zimekamatwa. Watuhumiwa waliokamatwa ni:-
1. MAJALIWA EDWARD [30] Mkazi wa Mwambene
2. EDSON KALINGA @ MANGI [32] Mkazi wa Iganzo
3. HAMIS ANYIMIKE [32] Mkazi wa Mafiati
4. ISSAH MWAMBELO [33] Fundi Magari na Mkazi wa Sae
5. KAMBELA HAMAD MWIPOPO [30] Mkazi wa Makunguru
6. GEORGE MWAKALOBO @ MWADADA [40] Mkazi wa Ipinda
7. MAJUTO SIMONI [37] Mkazi wa Kapwili
8. LWITIKO MWAIPOPO [38] Mkazi wa Ipinda
9. JAKOBO MWAKILEMA [47] Mkazi wa Ipinda
Watuhumiwa watafikishwa Mahakamani mara baada ya upelelezi kukamilika.