Na.Alex Sonna,Dodoma
Jeshi la Polisi mkoa wa Dodoma limefanya msako mkali katika Wilaya zote mkoani hapa na kufanikiwa kukamata Watuhumiwa 45 kwa kosa la kufanya biashara ya mafuta ya petrol na diesel katika makazi yao bila leseni ambacho ni kinyume cha sheria.
Akizungumza na Waandishi wa Habari Leo Sept.18,2019,Kamanda wa Polisi mkoa wa Dodoma SACP.Gilles Muroto amesema mafuta yaliyokuwa yakiuzwa ni aina ya Petrol lita 2118 na Diesel lita 2327.
SACP.Muroto amesema watuhumiwa hao walikamatwa katika maeneo tofautitofauti mkoani Dodoma ambapo walikuwa wakijihusisha na biashara hiyo bila vibali na katika mazingira hatarishi kwani huhifadhi na kuuza katika maeneo ya makazi na kuhatarisha maisha.
Kamanda Muroto ameainisha kuwa,katika Wilaya ya Mpwapwa wamekamatwa watu 7 waliokuwa wakiuza Petrol lita 70 pamoja na diesel lita 404,ambao ni Happiness Mtikwa [44] mkulima na mkazi wa Pwaga,Elizabeth Kululinda [20]mkulima mkazi wa wa Kimagai,Isaack Mtikwa [27]mfanyabiashara mkazi wa Pwaga,Richard Mchigani miaka [18] mkulima na mkazi wa Mwanakianga.
Wengine ni Michael Almasi [32],mkazi wa Godegode,Justin Letema [27]mkulima mkazi wa Kimagai,Ernei Fundi [28] na Mwingine ni Masta Kudeli[28]mkulima mfanyabiashara na mkazi wa Mang’angu.
Katika Wilaya ya Chemba kamanda Muroto amesema jeshi hilo limekamata watuhumiwa 5 waliokuwa wakiuza Mafuta ya Petrol lita 248, ambao ni Inbrahim Rajab [30],Rashid Ally Bakari [35],Fatuma Yusuph Mohamed [49],Juma Rajab[34] na Zubeda Ramadhan[30] wote wafanyabiashara na wakazi wa kijiji cha Hamai.
Wilaya ya Bahi amekamatwa mtuhumiwa mmoja Saul Lesaka miaka 21 mkazi wa kijiji cha Ibihwa alikiwa anafanya biashara ya mafuta ya petrol lita 640 katika makazi yao kitendo ambacho ni kinyume cha sheria.
Katika Wilaya ya Kongwa wamekamatwa watuhumiwa 8 wakiwa wanauza lita 80 ya petrol na diesel lita 730 ambao ni Samahani Chilingo [34]mkulima na mkazi wa Mbande,Festo Sailowa [22] mkazi wa Mbande,Emmanuel Jonas [27]mkulima na mkazi wa Mbande,Abdul Hamis [26]mkulima na Mkazi wa Kibaigwa ,Mushi Mushi [36]mkulima na mkazi wa Kibaigwa,Hatibu Omary Madudu [34] mkulima na Mkazi wa Banyibanyi na Shadrack Stephano[39] mkulima na Mkazi wa Banyibanyi.
Wilaya ya Chamwino wamekamatwa watuhumiwa 13 wakiwa wanauza mafuta petrol lita 587 na diesel lita 887 katika makazi yao ambao ni Stephano Kefa[29]mkulima na Mkazi wa kijiji cha Wilunze,Mateso Nzubesi [33] mkulima na mkazi wa kijiji cha Chalinze,Philemon Amos [32]mkazi wa kijiji cha Manchali,Ally Mohammed [35]mkazi wa Wilunze,Aman Msanga [42]mkazi wa Chinangali,Greyson Hotai [21]mkazi wa Maduma,Atanas Chigoji[22]mkazi wa kijiji cha Chamwino,
Wengine ni Issa Shamte [23]mkazi wa Kijiji cha Chamwino,Emmanuel Yared [22]mkazi wa Chamwino,Richard John [31]mkazi wa Chinangali,Peason Makasi [36]mkazi wa Chinangali,Musa Malogo [27]mkazi wa kijiji cha Msanga na Issa Msemo mkulima na Mkazi wa Msanga.
Katika Wilaya ya Kondoa wamekamatwa watuhumiwa 2 waliokuwa wakijihusisha na biashara ya mafuta katika makazi ya watu ambao ni Fami Juma Omary [22]mkazi wa Haubi na Aziz Hatibu [33] mkazi wa Pahi.
Wilaya ya Dodoma Waliokamatwa na Jeshi la polisi ni 7 wakiwa wanauza mafuta ya Petrol lita 45 katika makazi yao ambao ni Luka Lulambo[23]mkazi wa Chang’ombe,Khalid Hussein [42]mkazi wa Chang’ombe,Amina Seiph[37]mkazi wa Ndachi,Khalifa Ramadhan[45]mkazi wa Chang’ombe,Seiph Omary [44]mkazi wa Ndachi,Alshabih Issa[42]mkazi wa Itega na Daudi Kamwela [30]mkazi wa Chinangali.
Aidha Kamanda Muroto amesema Jeshi hilo limefanikiwa kukamkamata Happy Gidion [42] mkazi wa Kizota akiwa na Pombe haramu ya Moshi lita 8 na Misokoto 20 ya dawa za kulevya aina ya banghi kavu iliyosokotwa yenye ujazo wa nusu kilo.
Aidha, Jeshi la Polisi mkoani Dodoma limemkamata Emmanuel Jackson[35] mkazi wa Nkuhungu akiwa na seti moja ya kompyuta aina ya dell ambayo ni mali ya wizi akihifadhi na kumiliki pasipo na nyaraka za uthibitisho katika umiliki wake kinyume cha sheria.
Katika hatua nyingine Jeshi hilo limekamata Noti bandia zenye thamani ya zaidi ya Tsh.Milioni moja .