Afisa Maendeleo ya Jamii Mkoa wa Singida, Patrick Kasango akizungumza kabla ya kufunguliwa kikao cha kamati ya ulinzi wa wanawake na watoto Mkoa wa Singida kilichoketi jana Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Singida Mandewa. Kutoka kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Empower Society Transform Lives (ESTL) Joshua Lissu, Mwakilishi wa Mwenyekiti wa kamati hiyo, Buhacha Kichinda na Katibu wa Kamati hiyo, Shukrani Mbago.
Wajumbe wa kamati wakiwa kwenye kikao hicho.
Katibu wa Kamati hiyo, Shukrani Mbago akizungumza.
Mwakilishi wa Mwenyekiti wa kamati hiyo, Buhacha Kichinda akifungua kikao hicho.
Afisa Maendeleo ya Jamii Wilaya ya Singida, Veronica Mure akichangia jambo kwenye kamati hiyo.
Wafanyakazi wa ESTL wakiwa kwenye kamati hiyo.
Afisa Maendeleo ya Jamii kutoka Mkoa wa Singida, Jonathan Semiti akichangia jambo kwenye kamati hiyo.
Mkurugenzi Mtendaji wa ESTL, Joshua Lissu akiwasilisha mada.
Ngariba Mstaafu Hawa Njolo akizungumza.
Katibu wa Shirika la ESTL, Philbert Swai akizungumzia kuhusu Kituo cha Mkono kwa Mkono-One Stop Centre.
Wafanyakazi wa ESTL wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kikao hicho.
Wajumbe wa kamati ya ulinzi wa wanawake na watoto Mkoa wa Singida wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kikao hicho.
Na Dotto Mwaibale, Singida
SHIRIKA lisilokuwa la kiselikari la Empower Society Transform Lives ( ESTL) limetoa namba itakayotumika kutoa taarifa ya vitendo vya ukatili wa kijinsia na ukeketaji mkoani Singida.
Akizungumza katika kikao cha kamati ya ulinzi wa wanawake na watoto Mkoa wa Singida kilichoketi jana Hospitali ya Rufaa ya mkoa huo ya Mandewa Mkurugenzi Mtendaji wa shirika hilo Joshua Lissu alisema namba hizo zitasaidia wananchi kutoa taarifa za vitendo vya ukatili wa kijinsia na ukeketaji kwa usiri.
Alizitaja namba hizo kuwa ni 0710567003 na kuwa baada ya kupata taarifa hizo watazifuatilia na kuzitoa kwenye vyombo husika kama polisi na maeneo mengine kwa hatua za kisheria.
” Kutoa taarifa kwa kutumia namba hizo zitasaidia kutoa taarifa kwa usiri kwani kuna baadhi ya watu wanaogopa kwenda polisi kwa hofu ya kujulikana na wanaofanya vitendo hivyo na kuhatarisha usalama wao” alisema Lissu.
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Stars of Power Rescue Foundation (SPRF) Dk. Suleiman Mutani akizungumza wakati akitoa taarifa za utekelezaji wa mradi wa kutokomeza ukatili
huo Wilayani Ikungi unaofanywa na shirika hilo alisema ili kutokomeza vitendo hivyo ni lazima kuwepo na ushirikiano wa dhati baina ya mashirika hayo wananchi na vyombo vya
usalama kama polisi na mahakama.
huo Wilayani Ikungi unaofanywa na shirika hilo alisema ili kutokomeza vitendo hivyo ni lazima kuwepo na ushirikiano wa dhati baina ya mashirika hayo wananchi na vyombo vya
usalama kama polisi na mahakama.
Alisema bila ya ushirikiano huo bado kutakuwepo na changamoto ya kutokomeza vitendo hivyo licha ya kuwepo jitihada kubwa ya kupambana navyo zinazofanywa na mashirika hayo kwa kushirikiana na serikali.
Ngariba mstaafu ambaye ni mwezeshaji wa shirika la ESTL, Hawa Njolo alisema mafunzo na elimu yakitolewa kwa mangariba itakuwa ni njia pekee ya kutokomeza vitendo hivyo.
” Ikitolewa elimu kwa mangariba kuhusu madhara ya ukeketaji itasaidia kumaliza kabisa changamoto hii katika mkoa wetu na maeneo mengine hapa nchini” alisema Njolo.
Njolo alitumia nafasi hiyo kuwaomba mangariba wote kuacha kuendelea na ukeketaji na badala yake watubu na kuanza kufanya kazi zingine ili kuwanusuru watoto ambao ndio wahanga wakubwa wa vitendo hivyo.
Mtathimini wa mradi wa kupinga vitendo vya ukatili wa kijinsia kutoka Shirika la ESTL, Philbert Swai alisema mradi huo wa kutokomeza vitendo hivyo hasa ukeketaji umefadhiliwa na Shirika la The Foundation for Civil Society ambalo limetoa sh.milioni 60 kwa mwaka mmoja lengo likiwa ni kutoa mafunzo kwa makundi mbalimbali ya kijamii kwa ajili ya kutokomeza ukatili wa kijinsia na ukeketaji.