Mbunge wa Iramba Magharibi Mwigulu Nchemba akizungumza na wananchi waliojitokeza kwenye mkutano wa hadhara wakati akiwa katika ziara ya kikazi ya ukaguzi wa shughuli za maendeleo Jimboni humo, tarehe 17 Septemba 2019. (Picha Zote Na Innocent Natai, WazoHuru Blog)
Mbunge wa Iramba Magharibi Mwigulu Nchemba akisisitiza jambo wakati akizungumza na wananchi waliojitokeza kwenye mkutano wa hadhara wakati akiwa katika ziara ya kikazi ya ukaguzi wa shughuli za maendeleo Jimboni humo, tarehe 17 Septemba 2019.
Mbunge wa Iramba Magharibi Mwigulu Nchemba akisalimiana na wananchi waliojitokeza kwenye mkutano wa hadhara wakati akiwa katika ziara ya kikazi ya ukaguzi wa shughuli za maendeleo Jimboni humo, tarehe 17 Septemba 2019.
Mbunge wa Iramba Magharibi Mwigulu Nchemba akizungumza na wananchi waliojitokeza kwenye mkutano wa hadhara wakati akiwa katika ziara ya kikazi ya ukaguzi wa shughuli za maendeleo Jimboni humo, tarehe 17 Septemba 2019.
Mbunge wa Iramba Magharibi Mwigulu Nchemba leo
tarehe 17 Septemba 2019 amewataka wananchi kushirikiana katika ujenzi wa
maendeleo wa wilaya hiyo na kutumia vizuri vifaa vya ujenzi anavyozidi kuvitoa
katika wilaya hiyo ili kuwezesha maendeleo kukua na kutatua changamoto
zilizokuwa zikiwakabili, ameyasema hayo alipokuwa akikabidhi vifaa vya ujenzi
wakati wa ziara katika jimbo hilo.

Mwigulu alisema kuwa upo umuhimu wa kutunza vifaa
hivyo na kuvitumia vizuri katika shughuli zilizo elekezwa kwani kuna baadhi ya
watu wasio penda maendeleo wanaotumia misaada inayotolewa kwaajili ya shughuli
za maendeleo katika shughuli zao binafsi.

Aidha, aliongeza kuwa jimbo hilo limekuwa likikabiliwa
na changamoto ya baadhi ya shule kukosa mabweni na ukilinganisha kuwa zipo
mbali hivyo kuwa kadhia kubwa kwa wanafunzi jambo lililomfanya kuwa na mkakati
ikiwemo kutoa fedha na baadhi ya vifaa ili kuhakikisha angalau kila shule
inakuwa na mabweni kwa ajili ya kusaidia watoto wa kike wanaotoka umbali mrefu
na baadae kujengwa mabweni ya watoto wa kiume.

Alisema kuwa kwa wanafunzi kusomea majumbani ni
changamoto kwao kwani wanakosa muda kwaajili ya kujisomea na kujikuta wakiishia
kufanya shughuli za nyumbani ukiachilia mbali watoto wakike kupata ujauzito kwa
kubakwa au kudanganywa wakiwa njiani.

“Ninajitoa kuhakikisha naboresha huduma za elimu
kila kata na kila shule ili wanafunzi wetu ufaulu uongezeke sasa natoa onyo ole
wake kijana atakaemsumbua mtoto wa kike au kumpa ujauzito miaka 30 itakuhusu na
sina mchezo kwenye hili’’ Alisema Mwigulu.

Pia alibainisha kuwa amejipanga kuhakikisha anachangia
na kuhamasisha wananchi ili kuhakikisha anaboresha sekondari za kidato cha sita
katika wilaya hiyo kwa kushirikiana na wananchi hivyo amewaomba kutoa
ushirikiano.

Kadhalika, katika kuhakikisha huduma za afya zinapatikana
katika kila kijiji na kata alisema kuwa katika ziara hiyo atatoa baadhi ya
vifaa ili kusaidia kukamilisha zahanati ya Shelui ikiwemo saruji mifuko miamoja
na fedha taslimu milioni moja na nusu pia ameahidi kuhakikisha inakamilika kwa
wakati ili kuwasaidia wananchi kuondoa adha ya kukosa huduma za afya.

Awali, wakati wa kuanza ziara yake mapema
alishiriki katika makabidhiano ya msaada wa mabati 175 katika shule ya
sekondari Kinambeu kwa ajili ya kumalizia jengo la hosteli lililo ungua kwa
moto Septemba 2018 kutoka kwa NMB ambapo aliwashukuru kwa kuzidi kuisaidia jamii
na kumuunga mkono katika kuleta maendeleo kwenye jamii.

Mbunge huyo wa Jimbo la Iramba Magharibi Mhe
Mwigulu Nchemba ameendelea na ziara ikiwa ni siku ya pili ya ziara yake huku
ikishuhudiwa makundi ya mamia wakimlaki na kushiriki katika mikutano ya hadhara
anayoifanya katika kila kijiji, ziara hizo zinatarajiwa kuendelea tena kwa siku
mbili mfululizo.