WANGING’OMBE
Timu ya wakimbiza mwenge kitaifa ambayo inaongozwa na Mzee Mkongea Ally imegoma kuweka mawe ya msingi katika mradi wa tenki la maji wa Ilembula utakaogharimu zaidi ya mil 330 pamoja na mradi wa ujenzi wa jengo la ghorofa la ofisi za halmashauri utakaogharimu bil 2.7 hadi kukamilika kwa madai yakwamba imekuwa na disari kubwa katika utekelezaji wake.
Kufuatia mapungufu yaliobainika kiongozi huyo wa mbio za mwenge Mzee Mkongea Ally ametoa maagizo kwa taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa TAKUKURU kuondoka na nyaraka zote za utekelezaji wa mradi wa jengo ili kufanyia uchunguzi kwa kipindi cha wiki mbili na kisha kuwasilisha ripoti hiyo iliyobainika ili hatua za kisheria zikichukuliwe.
y
Awali akifafanua kuhusu miradi hiyo mkuu wa wilaya ya Wanging’ombe Comrade Ally Kassinge amesema ukiwa wilayani humo mwenge wa uhuru utakagua miradi 9 yenye thamani ya bil 1.9 kutoka sekta ya afya ,elimu na maji ambapo katika ufafanuzi imedaiwa kuwa miradi miwili itawekwa mawe ya msingi, minne kuzinduliwa huku mitatu ikikaguliwa.
Licha ya miradi yote iliyopaswa kuwekwa mawe ya msingi kugomewa na kiongozi wa mbio za mwenge kitaifa ,lakini miradi minne imezinduliwa na mingine mitatu kukaguliwa ukiwemo wa kituo cha afya cha Wanging’ombe na mradi wa ng’ombe hatua ambayo inawasukuma wananchi kutoa hisia zao.
Miradi mingine iliyokaguliwa ni mradi wa mabweni, mradu wa ng’ombe,kituo cha afya huku mingine ikiwa ni miradi ya klabu za utunzaji mazingira na rushwa katika shule ya sekondari Wanging’ombe na ile ya Mtakatifu Monica