Kaimu Mkurugenzi wa Benki ya NMB, Filbert Mponzi akimpongeza Rais wa Chama Cha Madaktari Tanzania Dk Elisha Osati baada ya kuzindua huduma ya AFYA LOAN uliofanyika katika Hospitali ya Heamed Bunju jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mkuu wa Kitengo cha Biashara wakubwa na wakati wa benki hiyo, Donatus Richard, Mkurugenzi Mkaazi wa Medical Credit Fund, Dk Heri Marwa na kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi ya Hospitali hiyo, Edwina Lupembe
Kaimu Mkurugenzi wa Beki ya NMB, Filbert Mponzi, Mkuu wa Kitengo cha Biashara wakubwa na wakati wa Benki hiyo, Donatus Richard (kulia), Rais wa Chama Cha Madaktari Tanzania, Dk Elisha Osati (wa tatu kutoka kushoto), Mkurugenzi Mkaazi wa Medical Credit Fund, Dk Heri marwa na Mwenyekiti wa Bodi wa Hospitali ya Heameda Edwina Lupembe wakifurahi baada ya kuzinduliwa kwa huduma ya AFYA LOAN.
Kaimu Mkurugenzi mtendaji wa Benki ya NMB, Filbert Mponzi akizugumza wakati uzinduzi wa huduma ya AFYA LOAN uliofanyika katika Hospitali ya Heameda iliyopo Bunju jijini Dar es Salaam.
*********************************
NA EMMANUEL MBATILO
Rais wa Chama cha Madaktari Tanzania (MAT), Dkt.Elisha Osati amewapongeza Nmb kwa juhudi ambazo wanazifanya za kuhakikisha sekta ya Afya hapa nchini inaboreshwa kuanzia katika huduma pamoja na vifaa tiba.
Ameyasema hayo leo katika uzinduzi wa utoaji mkopo kwa benki ya NMB kushirikiana na shirika la Stichting Medical Credit Fund (MCF) ambapo itatoa mikopo kuanzia Sh.Milioni 2 hadi Bil 5 wakati MCF inatoa dhamana ya ushirikiano kati ya Benki ya NMB asilimia 50 katika mikopo yote.
Akizungumza katika uzinduzi huo katika hosipitali ya Haemeda kwa lengo la kutoa mikopo ya gharama nafuu kwa hospitali binafsi, vituo vya afya na zahanati iliopewa jina la (NMB Afya loan), Dkt.Osati amesema kuwa Benki ya Nmb imefanya uwekezaji katika sekta ya afya hapa nchini hasa kujenga vituo vya afya vingi ambavyo vinawasaidia wananchi kupata huduma nzuri za kiafya.
Aidha amewataka NMB kuangalia uwezekano wa kuweka riba wezeshi ili kuwawezesha madaktari kupata mkopo ambao utawasaidia kuwekeza katika taaluma yao kuweza kuwasaidia wananchi kupata huduma ya afya bora.
Kwa upande wake Ofisa Mkuu wateja binafsi, biashara ndogo na za kati(NMB) Bw. Filbert Mponzi amesema, huduma hiyo ya mikopo imefika kwa wakati mwafaka na utachangia kuongeza upatikanaji wa huduma nafuu za afya na kujenga mifumo endelevu kwasababu upatikanaji wa mitaji unakuwa rahisi zaidi.
“Hii ni hatua nyingine kubwa kwa Benki ya NMB leo. Kuna fursa nyingi katika sekta ya afya nchini na sisi kama NMB, tumeliona hili na tumejikita kuwapa nafasi hospitali, vituo vya afya wasambazaji wa vifaa vya tiba kujiendeleza. Tunaimani huduma hii itachangia kwa kiasi kikubwa katika upatikanaji mkubwa wa utoaji huduma za afya za bei nafuu”.amesema Mponzi.
Naye Mkurugenzi wa shirika la Stichting Medical Credit Fund (MCF) Tanzania, Dk. Heri Marwa alisema kuanza utekelezaji wa huduma hiyo mpya ni muhimu katika kutimiza malengo ya MCF ya kuhakikisha watanzania wengi wapata huduma nafuu za afya na tiba.
“Upatikanaji wa mitaji kwa ajili ya uwekezaji ni changamoto kubwa katika nchi nyingi za Kiafrika na inazuia utoaji huduma nafuu za afya hususan tukiangalia mifumo endelevu ya afya.Kwa huduma hii tunafurahi kwamba hospitali nyingi binafsi, vituo vya afya vitapata na uwezo wa kuwekeza kwenye vifaa vya afya vya kisasa, na tunafurahi kushirikiana na benki bora nchini Tanzania kufanikisha upatikanaji wa mitaji ya biashara nchini,” Amesema Dk.Marwa.