Home Mchanganyiko ULEGA-UJENZI WA SGR NA KUFUFUA RELI YA ZAMANI UTAINUA SEKTA YA MIFUGO...

ULEGA-UJENZI WA SGR NA KUFUFUA RELI YA ZAMANI UTAINUA SEKTA YA MIFUGO NA KUMKOMBOA MFANYABIASHARA MFUGAJI KATIKA SOKO LA UHAKIKA

0

***************

NA MWAMVUA MWINYI,PWANI
NAIBU Waziri wa Mifugo na Uvuvi ,Abdallah Ulega ameeleza ,ujenzi wa reli ya kisasa ya standard gauge (SGR) pamoja na kufufuliwa kwa reli ya zamani, utainua sekta ya mifugo kwa kumpunguzia mfanyabiashara wa mifugo gharama za usafirishaji na upatikanaji wa soko la uhakika.
Aidha amebainisha kuwa, reli hiyo itakuwa sababu ya kubeba nyama ya kutosha kuingiza katika uwekezaji mkubwa wa kiwanda cha kuchakata mifugo na mazao eneo la Ruvu.
Akionyeshwa eneo litakaposhushwa mifugo kwenye reli mpya ya kisasa,na Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano mhandisi Atashasta Nditie ,naibu waziri huyo wa Mifugo na Uvuvi ,Ulega alisema reli hiyo ni chachu ya maendeleo na mkombozi kwa wafugaji.
Alieleza, wafugaji na wafanyabiashara wa mifugo wana gharama za kuweza kufikia masoko lakini mradi huu mkubwa wa usafiri wa reli unaenda kuweka historia kwa watanzania.
“Ombi ni kuhakikisha miundombinu ya reli ya zamani irejee katika mazingira yake na reli mpya kuzingatie mifugo na mazao “:SGR imewekewa mkazo na Rais dkt .John Magufuli ,itakuwa chachu ya kuinua sekta ya mifugo kuitoa Bara kuileta sokoni.”

Ulega ambae pia ni mbunge wa jimbo la Mkuranga alielezea, lengo jingine la ziara hiyo ni kutazama maendeleo ya ujenzi wa reli ya kisasa na kufunganisha na sekta ya mifugo,ya matarajio ya miundombinu ya reli hiyo kuwa rafiki kubebea mifugo .

Naye Nditie alisema, reli ya zamani iliharibika lakini kwasasa kupitia jitihada za serikali ya awamu ya tano imeshaanza kufufuliwa .
Alisema, wamepata mkopo nafuu fedha za Kimarekani milioni 300 kwa ajili ya kufufua reli hiyo na wameanza na maeneo korofi ili kuhakikisha mizigo yote iwe inapitia kwenye reli hiyo na baadae katika reli ya standard gauge.
Nditie alielezea, ikumbukwe kwamba reli hizo zinakwenda sambamba kwa asilimia 70.
Awali meneja mradi ,SGR LOTI, mhandisi Machibya Masanja alisema reli hiyo itakuwa na stesheni nne ikiwemo Soga,Pugu,Ruvu,Ngerengere na kituo cha mizigo na pia itakuwa mahsusi kwa ajili ya mifugo.
Akishukuru kwa niaba ya wafugaji, katibu wa chama cha wafugaji nchini ,Maghembe Makoe aliainisha kuwa miundombinu ya reli hiyo itatambua mifugo na kutatua changamoto za usafiri kwa mfanyabiashara wa mifugo.