Home Mchanganyiko Biteko – Kila mmoja atimize wajibu wake

Biteko – Kila mmoja atimize wajibu wake

0

Waziri wa Madini Doto Biteko akiwa kwenye Machimbo ya Madini ya
Viwandani eneo la Katoro.

Waziri wa Nishati Dkt Medard Kalemani akizungumza kwenye kikao
cha ndani na kamati ya ulizi na usalama Wilaya ya Bukombe chini ya
Mkuu wa wilaya hiyo Said Mtanda. Kulia kwake ni Waziri wa Madini
Doto Biteko.

Waziri wa Madini Doto Biteko kushoto na Waziri wa Nishati Dkt.
Medard Kalemani wa poli kushoto wakiangali jambo kwa mshangao
mkubwa.

Waziri wa Madini Doto Biteko akiwapungia mkono Wananchi wa
Bukombe mara baada mkutano wa hadhara Mjini Bukombe.

***********************************

Na Issa Mtuwa – Geita

Waziri wa Madini Doto Biteko amewataka Wachimbaji wa madini nchini
kutimiza wajibu wao kwakuwa serikali imeshatimiza na inaendelea kutimiza
wajibu wake kwa wachimbaji na wadau wengine wote katika sekta ya
madini.

Hayo ameyasema leo tarehe 14/09/2019 katika siku yake ya kwanza ya
ziara yake mkoani Geita wakati akiongea na wachimbaji wa madini ya
ujenzi eneo la Katoro.

Akiwa njiani kuelekea Bukombe Biteko aliongea na
wachimbaji hao kwa kuwasisitiza kulipa kodi ya serikali na tozo nyingine
kama sehemu ya kutimiza wajibu wao na kuunga mkono maamuzi ya Rais,
Dkt. John Pombe Magufuli aliewasikiliza kiliochao kuhusu utitiri wa kodi
zilizokuwa kero kwa wachimbaji na Rais kuamua kuziondoa.

Biteko amewaambia wachimbaji madini kote nchini kuwa, kwa sasa ni
zamu yao kutimiza wajibu kwa kulipa kodi, kuunga mkono jitihada alizo
zionyesha Rais Magufuli zilizopelekea mageuzi makubwa katika sekta
madini.
Wakati huo huo Biteko ambae pia ni Mbunge wa Bukombe ameungana na
Waziri wa Nishati Dkt. Medard Kalema katika kukagua utekelezaji wa ilani
ya chama tawala katika jimbo la Bukombe katika usambazaji wa umeme
kwa wananchi. Pamoja na kusikiliza kero za wana Bukombe kuhusu
Umeme Mawaziri hao wamejionea kusua sua kwa usambazaji wa umeme
na hatua iliyofikiwa jambo lililopelekea kung’olewa kwa Meneja wa Tanesco
wilaya ya Bukombe kwa kushindwa kutekeleza wajibu wake.

“Mhe. Kalemani leo mimi sina cha kuongea ujio wako wana Bukombe
wanasubiri kusikia kutoka kwako umeme utawaka lini, kwani wamekuwa
wakikuona kwenye vyombo vya habari mara Kilimanjaro, Mara Songea,
Mara Tanga ukipita ukiwasha umeme Wanabukombe nao leo wanapenda
wakuone ukiwasha umeme hapa kwao” alisema Biteko Mbunge wa
Bukombe huku akishangiliwa na umati mkubwa wa Wananchi wa
Bukombe.

Nae Waziri wa Nishati Dkt. Medard Kalemani alijibu mapigo ya mbunge wa
Bukombe kwa kutolea majibu kero zote zilizowasilishwa na Biteko kwa
niaba ya wananchi wake.

“Mhe. Waziri, kwanza nikupongeze kwa kazi kubwa na nzuri unayoifanya
kwa wananchi wako. Pili, nimekuja hapa mara mbili na leo mara ya tatu
maagizo niliyoyatoa awali naona hayajatekelezwa, sasa nasema hivii,
Meneja wa Tanesco wilaya ya Bukombe kuanzia sasa namfuta kazi sio
Meneja tena wa hapa Meneja wa Kanda tafuta kwa kumpeleka hapa lete
mwingine kesho”

“Pale sokoni kesho, nasema kesho, ipelekwe Transformer na jioni saa 10
umeme uwake kwenye maduka ya wafanyabiashara. Mkandarasi naagiza
ifikapo Desemba mwaka huu vijiji vyote 72 vya wilaya ya Bukombe viwe
vimesha unganishwa umeme. Mhe. Biteko mimi sijaja kukaa sana hapa
yangu ni hayo na kama haya yote niliyo yaangiza kwa kila jambo
yasipotekelezwa kwa tarehe zilizo pangwa nipigie simu” alisisitiza Kalemani
wakati wa mkutano wa hadhara na wananchi wa Jimbo la Bukombe.

Kwa upande mwingine Dkt. Kalemani amemsifu Mbunge wa Bukombe
ambae ni Waziri wa Madini kwa kutoa vifaa 250 bure vya kuunganishia
umeme huku kila kimoja kikigharimu Tshs. 300,000 kila kimoja itakacho
fungwa kwenye nyumba ya ukubwa wa chumba na sebule.

Biteko yupo kwenye ziara ya kikazi katika mikoa ya Geita, Kilimanjaro na
Kagera.