Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philipo Mpango,akizungumza wakati wa uzinduzi wa hafla ya ugawaji hati za ardhi, eneo la Ihumwa Ngaloni-Dodoma, kwa wanachama wa hazina SACCOS, tukio lililofanyika katika ukumbi wa Hazina jijini Dodoma.
Mwenyekiti wa Hazina SACCOS, Aliko Mwaiteleka,akitoa taarifa wakati wa uzinduzi wa hafla ya ugawaji hati za ardhi, eneo la Ihumwa Ngaloni-Dodoma, kwa wanachama wa hazina SACCOS, tukio lililofanyika katika ukumbi wa Hazina jijini Dodoma
Sehemu ya wanachama wakifatilia uzinduzi wa hafla ya ugawaji hati za ardhi, eneo la Ihumwa Ngaloni-Dodoma, kwa wanachama wa hazina SACCOS, tukio lililofanyika katika ukumbi wa Hazina jijini Dodoma
Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philipo Mpango,Hati yake wakati wa uzinduzi wa hafla ya ugawaji hati za ardhi, eneo la Ihumwa Ngaloni-Dodoma, kwa wanachama wa hazina SACCOS, tukio lililofanyika katika ukumbi wa Hazina jijini Dodoma.
Mwanachama akipokea hati yake katika ni waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philipo Mpango,akishuhudia tukio hilo wakati wa uzinduzi wa hafla ya ugawaji hati za ardhi, eneo la Ihumwa Ngaloni-Dodoma, kwa wanachama wa hazina SACCOS, tukio lililofanyika katika ukumbi wa Hazina jijini Dodoma.
Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philipo Mpango,akiwa katika picha ya pamoja na wanachama mara baada ya kuzindua hafla ya ugawaji hati za ardhi, eneo la Ihumwa Ngaloni-Dodoma, kwa wanachama wa hazina SACCOS, tukio lililofanyika katika ukumbi wa Hazina jijini Dodoma.
…………………….
Na.Alex Sonna, Dodoma.
Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philipo Mpango, amezitaka benki na taasisi nyingine za kifedha kuangalia upya namna ya kukokotoa viwango vya riba wanavyoviweka katika mikopo wanayoitoa kwani ni viwango vya juu na haziwanufaishi wanaokopa na kuwa sio msaada tena.
Pia ameitaka Banki kuu ya Tanzania BOT kuzifanyia utafiti benki zote na taasisi za kifedha kama zinazingatia vigezo hasa katika riba wanazotoza kwa wanachama wao na zinafuata utaratibu uliowekwa.
Waziri Dkt. Mpango, ameyasema hayo leo Jijini Dodoma wakati akizindua hafla ya ugawaji hati za ardhi, eneo la Ihumwa Ngaloni-Dodoma, kwa wanachama wa hazina SACCOS, tukio lililofanyika katika ukumbi wa Hazina Dodoma.
Dkt. Mpango amesema amekutana na benki moja ambayo inatoa mikopo kwa watumishi kwa riba ya asilimia 32, na alipowauliza na wao wakasema wanachukua mikopo hiyo katika benki nyingine kwa riba ya asilimia 20, jambo ambalo riba hiyo ni kubwa sana.
“Ni jana tu nimekutana na benki hiyo na kukuta inatoa riba kwa asilimia 32 na nilipowadodosa wakanijibu na wao wanachukua mikopo hiyo benki nyingine kwa asilimia 20, lakini hii ya asilimia 20 bado ni kubwa sana, niitake benki kuu kutafiti hivi viwango vya riba kwa mabenki yote na taasisi zote za kifedha” amesema Dkt Mpango.
Aidha amekipongeza kikundi cha Hazina SACCOS, kwa kupima maeneo na kupata viwanja kwa ajiri ya wanachama wake, kwani jambo hilo ni kuunga mkono serikali katika kuendeleza makao makuu ya nchi na kuendeleza Jiji la Dodoma.
Pia amewataka watumishi wa serikali kuchangamkia fulsa kwa kujiunga na chama hicho cha ushirika hazina SACCOS, ili kama watumishi wa serikali waweze kunufaika na mikopo ya bei nafuu inayotolewa na hazina SACCOS, na kukitaka kikundi hicho kuzingatia maadili na kuepuka ubadhilifu.
Waziri Dkt Mpango amemtaka mlezi wa hazina SACCOS, ambaye ni katibu mkuu wa Wizara hiyo, Dotto James, kuketi meza moja na Mkurugenzi mkuu wa shirika la reli Tanzania(TRL) Masanja Kadogosa, kama wamemaliza suala la kupima eneo yanayopitiwa na reli ya kisasa ili watumishi wenye viwanja maeneo hayo waanze kuviendeleza.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Hazina SACCOS, Aliko Mwaiteleka, amesema chama hicho kilianzishwa mwaka 1973, na waliokuwa wafanya kazi wa Wizara ya Fedha, na baadaye kusambaa, na kina wanachama zaidi ya elfu tano mia sita(5600), na kinajihusisha na utoaji wa mikopo ya bei nafuu na kina akiba ya shilingi bilioni nane(8).