Bondia Juma Choki akipima uzito kwa ajili ya mpambano wake na Emanuel Mwakyembe utakaofanyika katika ukumbi wa Backet Lounger Septemba 15 kushoto ni katibu wa Kamisheni ya ngumi Tanzania TPBRC Yahya Pori.
Kocha wa kimataifa wa mchezo wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila Super D kushoto akiwa katika picha ya pamoja na Jumachoka na kocha Edward Lwiyakwipya na bondia Emanuel Mwakyembe.
*****************************
NA Mwandishi wetu
MABONDIA Juma Choki na Emanuel Mwakyembe wamepima uzito kwa aqjili ya mpambano wao kwa ajili ya mpambano wa King Of The Ring utakaofanyika Septemba 15 katika ukumbi wa Backet Lounger uliopo Masaki Dar ES salaam
Mabondia hawo wamefanikiwa kufika Fainal baada ya kuwashinda wapinzani wao katika hatua za awali mshindi katika mpambano huo atanyakuwa pikipiki pamoja na kitita cha shilingi laki tano na atakaepigwa atachukuwa flat TV kubwa pamoja na kitita cha shilingi laki tano
Promota wa Mpambano huo Crisiani Kisinini amesema kuwa mbali na mpambano uho kutakuwa na mapambano mengine ambapo bondia Issa Nampepeche atazipiga na Emanuel Timtimu na mabondia wengine wengi
Aliongeza kwa kusema kuwa mapambano ya ngumi yataanza saa moja kamili usiku uki kila likipigwa pambano moja kunakuwa na burudani na mpambano wa mwisho kabisa utafanyika saa tano na saa sita itakuwa mwisho na atajulikana nani ni champion wa mashindano ya King Of The Ring ambapo Mshindi wa kwanza mpaka wa tatu watajinyakulia zawadi kubwa
Mshindi wa kwanza ataondoka na Pikipiki pamoja na laki tano pesa taslim na wa pili atajinyakulia flat TV kubwa pamoja na Laki tano wa tatu atachukuwa kiasi cha pesa Taslim shiling Laki Tano
Hivyo amewataka wapenzi wa mchezo wa masumbwi waje waangalie nani bingwa katika uzito wa KG 58 kwa hapa nchini Tanzania