Home Mchanganyiko  WAZIRI LUGOLA AMUONYA MUSIBA KUUAMINISHA UMMA KUWA ANATUMIWA NA SERIKALI

 WAZIRI LUGOLA AMUONYA MUSIBA KUUAMINISHA UMMA KUWA ANATUMIWA NA SERIKALI

0

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe Kangi Lugola akizungumza na wandishi wa habari (hawapo pichani) ofisini kwake jijini Dodoma kuhusu hali ya kiusalama nchini

………………

Na.Alex Sonna,Dodoma

Waziri wa Mambo ya ndani ya Nchi Mhe.Kangi Lugola amemtahadharisha na Kumwonya Mwanaharakati huru  Cyprian  Musiba kuacha kuwaaminisha watanzania kuwa Serikali inamtumia.

Hayo ameyasema jijini Dodoma Wakati akizungumza na Waandishi wa Habari ofisini kwake amesema kuwa Mwanaharakati Cyprian Musiba   serikali haimtumii na mambo yake hayabarikiwi na Serikali   bali ni matakwa yake binafsi.

“Kuna mwanaharakati huru Musiba anawadanganya watanzania kuwa serikali ina mtumia mpaka baadhi ya viongozi mbalimbali na Watanzania inafikia hatua ya kumwogopa,nataka kuwafahamisha watanzania serikali haimtumii endapo ataendelea kujigamba namna hiyo serikali itamchukulia hatua za kisheria”Amesema Lugola.

Lugola  amesema kuna baadhi ya Watanzania wakiwemo viongozi mbalimbali wamekuwa wakiaminishwa na Mwanaharakati huyo kuwa serikali inamtumia   ambapo amesema hayo ni maneno yasiyokuwa ya kweli.

Hivyo Serikali kupitia Wizara ya Mambo ya ndani imesema endapo Mwanaharakati huru Cyprian Musiba ataendelea kuvuka mipaka kwa kuwaaminisha watanzania kuwa  anatumiwa   na serikali ,serikali itamchukulia hatua   kali za kisheria.

Hata hivyo Aidha,Lugola amewatahadharisha  baadhi ya watu ambao wamekuwa wakitumia majina ya viongozi na Mitandao kutapeli watu wengine ambapo amesema Serikali imejipanga kukabiliana na tatizo hilo.

.