Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Kusimamia Ofisi za Viongozi Wakuu wa
Kitaifa ya Baraza la Wawakilishi la Zanzibar hiyo Mhe. Ali Selemani Ali
akizungumza mbele ya wajumbe wa Kamati hiyo na viongozi mbalimbali
walipofika katika eneo walilokabidhiwa.
Wajumbe wa Kamati ya Kusimamia Ofisi za Viongozi Wakuu wa Kitaifa ya
Baraza la Wawakilishi la Zanzibar wakikagua eneo walilokabidhiwa na Serikali ya
Jamhuri ya Muungano.
Wajumbe wakiangalia ramani ya eneo hilo walilokabidhiwa kutoka kwa mtaalamu
wa ardhi.
Wajumbe wa Kamati ya Kusimamia Ofisi za Viongozi Wakuu wa Kitaifa ya
Baraza la Wawakilishi la Zanzibar wakikagua eneo walilokabidhiwa na Serikali ya
Jamhuri ya Muungano.
Muonekano wa sehemu ya eneo la Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar
watakakalijenga Ofisi zake walilokabidhiwa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania Jijini Dodoma.
**************************
Wajumbe wa Kamati ya Kusimamia Ofisi za Viongozi Wakuu wa Kitaifa ya
Baraza la Wawakilishi la Zanzibar wametembelea kiwanja kwa ajili ya kujengwa
Ofisi za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) katika eneo la Mahoma Makulu
Jijini Dodoma.
Ziara hiyo pia ilihusisha wataalamu kutoka Serikali hiyo na viongozi mbalimbali
akiwemo Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Pili wa Zanzibar Mhe. Mihayo Juma
Nhunga ambaye aliishukuru Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa
kuwakabidhi pa kiwanja hicho.
Mhe. Nhunga alisema kuwa SMZ inafarijika kupata kiwanja hicho ambacho kina
ukubwa wa hekta 30 na kuwa itaanza haraka ujenzi wa izo uhusiano wa pande
mbili za Muungano utaendelea kuimarika.
Serikali hizi mbili zina uhusiano na ushirikiano mzuri na tunaona namna Serikali
ya Jamhuri ya Muungano ilivyojitoa na kutupatia kiwanja hiki na tunaona thamani
ya Dodoma sasa tofauti na zamani hivyo tunaanza haraka ujenzi wa ofisi zetu
tuhamie hapa," alisema.
Kwa upande wake Makamu Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mhe. Ali Selemani Ali
wanashukuru kwa kupata ardhi hiyo na kuwa ina thamani kubwa kwa Serikali ya
Zanzibar hivyo undugu baina ya pande hizo mbili utaendelea kuimarika.
Mhe. Ali aliahidi kuwa kama Kamati wataishauri SMZ kuanzisha ujenzi wa Ofisi
za serikali hiyo kwa kasi ili waweze kuhamia na kuanza shughuli zake katika Jiji
la Dodoma.
Akitoa shukrani zake kwa ujumbe huo Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa
Rais Balozi Joseph Sokoine aliyeambatana na wakurugenzi wa Idara ya
Muungano aliwakarisha kuanza ujenzi na kuhamia.
Balozi Sokoine alisema kuwa kukamilika kwa ujenzi wa Ofisi za Serikali ya
Mapinduzi Zanzibar kutaimarisha Muungano na undugu baina ya wananchi wa
pande hizo mbili.
“Tunafarijika sana tunapoona mnafika hapa kwenye kiwanja chenu mara kwa
mara na kuona namna mtakavyoanza ujenzi na kukamilika kwa Ofisi hizi kutaleta
ushirikiano mzuri baina yetu sote”. Alisema.